Rayvanny anunua gari la kifahari kwa Tsh254m

Muhtasari

•Rayvanny alionyesha gari lake jipya kupitia kanda ndogo ya video ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

•Baba Levo alimchana Harmonize kwa kuandika jina la mpenzi wake wa zamani, Kajala Masanja kwenye Range Rover huku akidai kuwa ni kiki tu na gari hilo sio lake.

Image: HISANI

Staa wa Bongo Raymond Shaban Mwakyusa almaarufu Rayvanny ni mmiliki mpya wa gari la kifahari aina ya V8.

Rayvanny alionyesha gari lake jipya kupitia kanda ndogo ya video ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kulingana na mwanadani wake na mwanamuziki mwenzake Baba Levo, gari hilo lilimgharimu Rayvanny Tsh 254,000,000. (Ksh13M)

"Kitendo cha kuhama kutoka kwenye Prado ya milioni 80 kwenda kwenye Brand New V8 ya milioni 254 unastahili pongezi mdogo wangu Rayvanny," Baba Levo alisema kupitia Instagram.

Wakati huo huo, Baba Levo alimchana Harmonize kwa kuandika jina la mpenzi wake wa zamani, Kajala Masanja kwenye Range Rover huku akidai kuwa ni kiki tu na gari hilo sio lake.

"Wakati Kilandage anatengeneza kiki kwa kuandika magari ya watu majina ya mademu, Rayvanny amenunua Brand New V8 yaani mpyaa," Alisema.