Heri kuwa peke yako kuliko kuwa na mtu asiyekufaa-Fridah Kajala kamjibu Harmonize?

Muhtasari
  • Harmonize alianza kuashiria dalili za kumpeza Kajala takriban mwezi mmoja uliopita hata kabla ya kutangaza utengano wake na Briana Jai
Harmonize na Kajala Masanja
Harmonize na Kajala Masanja
Image: HISANI

Msanii wa bongo Harmonize kwa siku chache zilizopita amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kuomba aliyeuwa mpenzi wake Fridah Kajala amrudie.

Msanii huyo alizidi na kumnunulia Kajala zawadi za kuonyesha kwamba alimkosea na anajutia kwa yale alimtendea.

Harmonize alianza kuashiria dalili za kumpeza Kajala takriban mwezi mmoja uliopita hata kabla ya kutangaza utengano wake na Briana Jai.

Hapo awali, Harmonize alifichua hali ya kumpeza Kajala na ukweli kwamba bado anampenda kulichangia katika kuachana kwake na Briana.

"Hatuko pamoja na Briana sababu moja nilimwambia nimetengana na mtu bila kugombana na nampenda sanaa sasa sina uhakika kama nimemove on, lolote linaweza kutokea,"Harmonize alisema.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Harmonize aliweka bango lake na mwigizaji huyo katika eneo la Kinondoni. 

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisema bango hilo lenye maandishi 'Lovers' lilimgharimu shilingi milioni 12  za Tanzania. (Ksh 600,000)

"Niliweka mimi 100%. Nilitumia milioni 12. Itakuwa pale kwa takriban miezi sita," Harmonize alisema.

Mapema mwezi Aprili, mwanamuziki huyo alienda katika duka la vito na kutambua mkufu wa thamani ambao Kajala aliokuwa ameupenda Kajala.  Harmonize alifichua alitumia shilingi milioni tano za Tanzania kupata cheni hiyo.

"Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu unayependa. Wakupeleka sasa? 5M kwa dhahabu," Alisema Harmonize.

Hata baada ya haya yote Kajala hakusema neno moja kuhusu mambo ya Harmonize.

Siku ya JUmapili Kajala aliandika ujumbe ambao wanamitandao wengi wamedai kwamba alikuwa anamjibu msanii huyo.

Kajala alibaini kuwa heri mtu kuishi peke yake kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyemfaa.

"Mfano mwema wa heri kuwa peke yako kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyekufaa," Kajala Aliandika.