Jux - Kupendeza na kupenda magari mazuri ni kitu nilirithi kutoka kwa baba

Muhtasari

• Msanii Juma Jux alisema kwamba mitindo yake ya kifasheni na kupenda magari mazuri ni kitu alichorithi kutoka kwa babake mzazi.

Juma Jux
Jux, Gykie Juma Jux
Image: Instagram

Mwanamuziki na mjasirimali ambaye pia anajiongeza kama mwanamitindo wa kiume Juma Jux ameweka wazi kwamba kupendeza kwake na mapenzi yake ya dhati kwa fasheni si kitu cha kushtukiza tu maishani mwake bali ni hulka ambayo aliirithi kutoka kwa babake mzazi.

Jux alieleza kwamba hata mtindo wa kutaka kununua na kumiliki magari mazuri ni kitu alichokirithi kutoka kwa mzee wake.

"Mzee wangu alikuwa msafi sana, anajipenda, anaendesha mipira mikali (magari mazuri) nini, kule Lumumba alikuwa anaingiza magari makali anauza.Nakumbuka hata magari yaliyokuwa yanakuja nyumbani kwetu kipindi hicho ni magari makali, yaani ni mzee alikuwa na mipira tu mikali," amesema na kuongeza.

Alisema kwamba alipenda sana kuona baba yake akiingiza magari mazuri aina ya Mercedes Benz na kujisemea kimoyomoyo kwamba ipo siku tu atakuja kuyanunua na pengine kuyamiliki na hilo linampa msukumo fulani wa kuchakarika maishani ili kutimiza azma yake ya kufuata nyayo za mzee wake ambaye sasa ni marehemu.

"Nikasema siku moja nitakuja kuinunua (Mercedes Benz), Baba yangu amefariki muda kidogo, so popote alipo atakuwa anajivunia ninaimiliki sasa"

E-Plus