Kwisha! Penzi la Rayvanny na Kajala lakata kamba na kuzama

Muhtasari

• Fununu kutoka Tanzania ni kwamba msanii Rayvanny na mpenzi wake Paula Kajala wameachana.

• Wawili hao wamesitisha kufuatana kwenye mtandao wa YouTube na kufuta picha zote za pamoja.

Rayvanny na Paula Kajala
Image: Hisani

Fununu zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ni kwamba penzi kati ya msanii Rayvanny na mpenzi wake Paula kajala limekata Kamba baada ya misukosuko ya muda mrefu.

Inasemekana hatimaye wawili hao wametengana, picha kufutwa na kuacha kufuatana kwenye mtandao wa Instagram ambapo sasa ukitazama vizuri katika orodha ya watu anaowafuata Rayvanny, Paula hayupo pale hali ya kuwa siku za nyuma alikuwa miongoni mmwa watu waliokuwa wakifuatwa na msanii huyo.

Kwa upande wa mwanadada huyo pia ni vivyo hivyo ambapo baada ya kuenda masomoni Uturuki, Rayvanny alikuwa mpweke sana na pengine ndio sababu ya kulitamatisha penzi lao.

Juzi kati Rayvanny aliungana na aliyekuwa mpenzi wake Fahyvanny kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe ambapo wapenzi hao wa zamani walimsherehekea kwa msururu wa picha safi na jumbe maalumu.

Penzi la Rayvanny na Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji mkongwe Fridah Kajala liliwekwa wazi baada ya uvumi kuibuka kwamba msanii Harmonize alikuwa akimvizia binti huyo kipindo hicho akiwa bado na mahusiano ya kimapenzi na mamake Fridah Kajala.

Wadau kama vipi hapa Fahyvanny ameamua liwe liwalo penzi la Rayvanny lazima lirudi Tanga, chimbuko la mapenzi lenyewe.