Shabiki mmoja amewatupia cheche kali wasanii ambao mara kwa mara wanasema kwamba wameingia katika depression.
Kulingana na mwanaume huyo, wasanii wengi hutumia pesa zao katika starehe badala ya kuwekeza katika miradi itakayowafaidi.
" Hakuna kitu kama depression, ukipata pesa kidogo ushaanza kupiga gym Kilimani ati umefika," alisema.
Alishikilia kwamba mastaa wengi sasa wamefanya mazoea ya kuomba mchango kila mara wanapokuwa na changamoto, akisema kwamba ni mwiba ambao wanajidunga wenyewe.