Wakati Diamond yupo Ulaya kikazi, Harmonize anakimbizana na Kajala, akifeli atasema karogwa, huo ni ushamba!

Muhtasari

• Harmonize amesutwa kwa kukimbizana na wanawake (Kajala) wakati wenzake kama Diamond wapo Ulaya kupiga shughuli za kimuziki.

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Screengrabs: YouTube

Hivi unajua tofauti kubwa baina ya wasanii Diamond na Harmonize, haswa katika kipindi hichi ambapo wengi wanajaribu kuwafananisha wawili hao kutoka mafanikio kimuziki, maisha, fasheni na utajiri?

Wengi wanajiuliza mbona msanii Diamond ametia fora sana katika kutawala Sanaa ya bongo kimuziki kwa miongo kadhaa bila kufifia kama wenzake walioanza nao, lakini je, wamewahi jiuliza ni nini kinamfanya mwanamuziki huyo kuzidisha umaarufu wake kutoka kwa vizazi vya jana hadi vizazi vya leo?

Majibu yote haya utayapata katika Makala fulani ambayo yameandikwa na mdau kwa jina Hope Tyga kuhusu ni kwa nini itamgharimu Harmonize muda mwingi wa kujifunza kutoka kwa Diamond ili kumfikia katika ufanisi.

Kulingana na Tyga, wakati Diamond ameelekea Ulaya katika shughuli rasmi za kikazi kimuziki, mwenzake aliyekuwa anapigiwa upato kumrithi bado yupo nyumbani anazidi kulilia mapenzi na kumfuata mwanamke ambaye hamtaki, nazungumzia Harmonize akizidi kumfuata Kajala Masanja kumrudia kimapenzi.

“Vijana fanyeni kazi! Bila kazi hakuna maendeleo. Diamond ni kijana mchapakazi, hanaga muda wa kupoteza, kila kitu kinachotokea mbele yake, yeye hugeuza kuwa fursa.

Tunaona hivi sasa Diamond yupo Bara la ulaya, hajaenda kwaajili ya kutalii, ameenda kikazi zaidi, tunaamini safari yake hii italeta faida kubwa katika muziki wake na biashara zake kwa ujumla. Wakati Diamond akipambana huko ulaya tunamuona Harmonize akiwa hapa Bongo anapoteza muda tu, yeye kila siku ni kulialia tu, mara aombe msamaha kwa Kajala, ni vituko tu,” aliandika mdau Tyga.

Tyga anazidi kumtaka Harmonize kujichuna masikio na kuachana kukimbizana na wanawake kwani hayo ni mambo ya kupita tu na badala yake kuelekeza muda wake mwingi katika kuipalilia nyota yake kwani asipofanikiwa atasahau kwamba hakutia bidi na kusingizia ulozi.

“Badae Harmo asipofanikiwa atalaumu kwamba anarogwa, wakati ukweli unaonesha kabisa kijana sio mchapakazi, yeye anawaza wanawake tu, hana anachowaza zaidi. Mwenzake kalamba ubalozi wa Airtel, yeye hajapata hata ubalozi wa chaki,” Tyga alimalizia kutema lulu.

Unahisi ushauri huu ni maridhawa na wa kutiliwa mkazo na Harmonize ama ni chuki tu na vita kijana anapigwa?