'Nilikuwa napitia wakati mgumu,'Nandy asema baada ya kurejesha akaunti yake iliyokuwa imedukuliwa

Muhtasari
  • Hizi majuzi msanii maarufu Nandy alitangaza kwamba akaunti yake ya instagram iluyona zaidi ya mashabiki milioni moja imedukuliwa na watu asiowajua

Stori za wasanii kudukuliwa akaunti zao za Instagram hazijaanza leo, utakumbuka kwamba mwaka 2015 tatizo kama hilo liliwahi kumkumba msanii Fid Q na Shilole, Linah (2016) na Mkenya Sanaipei Tande (Feb 2021).

Hizi majuzi msanii maarufu Nandy alitangaza kwamba akaunti yake ya instagram iluyona zaidi ya mashabiki milioni moja imedukuliwa na watu asiowajua.

Nandy siku ya Jumatano alisema kwamba akaunti yae imerejeshwa, huku akizungumza baada ya hayo alisema kuwa ilikuwa vigumu kwake kuweka tabasamu usoni mwake au kwa anaowapenda.

Pia msanii huyo alimshukuru mpenzi wake kwani alikuwa tayari kumpa akaunti yake ili aendelee na kazi yake.

"Haikuwa rahisi kuweka smile Kwenye nyuso za watu wangu wa karibu while nilikuwa napitia wakati mgumu… hii account ni NUSU ya mafanikio yangu ya mziki! Shukrani za dhati kwa TCRA @tcra_tanzania na business partners wangu @empawaafrica bila kumsahau kipenzi changu @billnass masikini ulikuwa uko tayar kabisa kuniachia account yako ili tu niweke amani na furaha Kwenye uso wangu Nakupenda sana na ASANTE kwa kuwa na mimi kwa kipindi hichi!Nisiseme Mengi KAZI IENDELEEEE 💪," Alisema Nandy.