Fahamu Kajala kwa undani: Alikuwa na ndoto ya kuwa 'sister', aliwahi fungwa jela mwaka mmoja...

Muhtasari

• Kajala alifungwa mwaka mmoja jela kwa kuuza nyumba na mumewe, nyumba iliyokataliwa kisheria kuuzwa.

• Alikuwa na ndoto ya kuwa mtawa wa Kikatoliki japo. Alikuwa mraibu wa vileo japo kwa sasa hatumii kileo hata chembe.

Kajala Masanja Frida
Kajala Masanja Frida
Image: Instagram

Kwa muda mrefu sasa, Harmonize amekuwa akizungumziwa sana mitandaoni kuhusu Sakata lake la kuamua kutangaza penzi lake wazi kwa mwanamama Frida Kajala huku akimtaka amrudie na kumsamehe waishi kama zamani, lakini je, watu wengi wanamfahamu Kajala kando na kumjua wakati akiigiza na wakati ameingia kwenye penzi na Harmonize mwaka mmoja uliopita?

Kwa wale wasiomfahamu mwanamama huyu, leo mtapata firsa ya kufahamu japo machache kumhusu kutoka maisha yake binafwsi, maisha yake kama muigizaji, ndoa ya awali iliyovunjika, mahusiano yake na msanii Harmonize miongoni mwa mengine.

Kwa taarifa zilizopo kwenye meza ya umma ni kwamba mwanamama huyu ana umri wa miaka 39 na jina lake halisi ni Winfrida Kajala Masanja.

Kajala alimpata mwanawe Paula Kajala akiwa na umri wa miaka 19 tu, Paula ambaye kwa sasa yuko nchini Uturuki kwa shughuli za masomo. Kutokana na kupata ujauzito akiwa naumri mbichi huo, Kajala hakubahatika hata kumaliza elimu ya kidato cha nne.

Inasemekana kwamba Kajala alianza utundu akiwa na umri mdogo sana ambayo alikuwa akitoweka nyumbani kwa siku kadhaa na kurudi baadae, licha ya kuwa wazazi wake wote walihudumu kama polisi na ambao kwa sasa wamestaafu.

Unaambiwa Kajala alikuwa na ndoto kubwa sana enzi za utotoni. Ndoto yenyewe alikuwa anataka kuwa mtawa wa Kikatoliki. Ndoto hii ilimuona Kajala akifuata masono ya utawa hadi kwenye shule ya kimishonari lakini kwa bahati mbaya ikabidi asitishe masomo hayo kutokana na sababu za kiafya.

Kajala aliwahi olewa na mwanaume kwa jina P-Funk Majani lakini ndoa hiyo haikudumu kutokana na kwamba mwanaume huyo kila mara alikuwa akimgeuza Kajala mpira wa kitenesi na kumdunda sana.

Nani kasema eti watu hawabadiliki na kuasi tabia zao mbaya za ujanani? Licha ya kuwa mtiribu na mraibu wa vileo wa kupigiwa mfano enzi za ujana wake, Kwa sasa Kajala hatumii kileo chochote.

Mwanamama huyo aliwahi hukumiwa kifungo cha mwaka 1 jela kwa kushirikiana na aliyekuwa mumewe kuuza nyumba yao ambao kisheria ilikuwa imepigwa marufuku kunadiwa kwqa ridhaa ya mke wa awali wa jamaa huyo. Rafiki yake wa karibu, Wema Sepetu alimtolea dhamana ya laki sita na elfu 46 pesa za Kenya ambazo ni sawa na milioni 13 pesa za Kitanzania, na kumtoa jela. Kitendo hicho kilimfanya Kajala kuchora tattoo ya Wema ambayo ako nayo mpaka sasa.

Kwa sasa Wema na Kajala hawako katika uhusiano mwema licha ya kumtolea dhamana kutoka jela.

@Hopetygatz