"Harmonize kumfikia Diamond, aah bado sana!" - Baba Levo

Muhtasari

• Baba Levo - “Nishasema Mtu yeyote atakaejaribu Kushindana na Diamond Ataishia Vitu Vingi,”

Harmonize, Baba Levo, Diamond Platnumz
Harmonize, Baba Levo, Diamond Platnumz
Image: Instagram

Msanii na mtaalamu wa ujenzi Baba Levo amemchamba Harmonize kwa mara nyingine tena na kusema kwamba mkurugenzi huyo wa Konde Music Worldwide hana uwezo hata chembe kumzima Diamond Platnumz kwa lolote iwe kimuziki au hata kufanya kiki.

Kulingana na Baba levo, Harmonize bado hajai hata kwenye kiganja cha Diamond kwani ni kama mtoto tu anayejaribu kuiga babake wa muziki lakini ameshindwa na kuamua kutumia njia hasi ya kutembeza chuki na matusi dhidi yake mitandaoni badala ya kujitahidi kumfikia na akishindwa kumfikia basi arudi kujiunga naye kumshabikia.

“Harmonize Hana Uwezo wa kutengeneza Kiki ya Kumfunika Diamond Platnumz, Kwa Vyovyote Vile Hana Uwezo wa Kuzima EP ya FOA,” Baba Levo alisema.

Chawa huyo wa Wasafi pia alizidi kutilia mkazo kwamba amesema mara nyingi tu kwamba si Harmonize pekee bali msanii yeyote atakayedanganyika kuchukua mkondo wa kujaribu kushindana na Diamond basi atapoteza vingi, yaani itakuwa kama ng’ombe anayejaribu kushindana na ndovu kunya, bila shaka atakwama kwenye gogo la tembo.

“Nishasema Mtu yeyote atakaejaribu Kushindana na Diamond Ataishia Vitu Vingi,” alisisitiza kutoa onyo hilo Baba Levo.