Nimeachwa niko single-Akothee asema, ukweli au ni kiki?

Muhtasari
  • Akothee ni miongoni mwa wasanii maarufu nchini na washawishi wakubwa katika mitandao ya kijamii
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Akothee ni miongoni mwa wasanii maarufu nchini na washawishi wakubwa katika mitandao ya kijamii.

Msanii huyo anafahamika sana mitandaoni kutoka na maisha yake anayoishi, na jinsi anavyowapenda watoto wake.

Uhusiano wa kimapenzi kati ya Nelly Oaks na Akothee, ulipokelewa na hisia tofauti na wanamitandao, kwani wengi walidai kwamba Akothee ni mzee kulio mpeni wake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Ijumaa Akothee aiandika ujumbe na kudai kwamba ameachwa.

"Niamchwa Imagine,niko single tena hii relationship usichukulie personal," Aliandika Akothee.

Aliongeza;

"Mnakumbuka nilivyowaambiwa ninamchumba hadi pale kifo kitatutenganisha, haya basi amekusanya virago na kuenda, niko single tena watu wangu, barabara ya uhusiano kawaida inakuanga ikijengwa."