Akothee afunguka kuhusu madai kuwa ameachwa na mpenziwe Nelly Oaks

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa mahusiano yake na Oaks bado yapo imara na kuwakosoa wale walioamini madai hayo.

•Hapo awali Akothee alikuwa amedai kwamba yupo single tena baada ya "mpaka kifo kitakapotutenganisha" kumwacha.

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Mwanamuziki Akothee amejitokeza kuweka wazi kwamba madai yake ya Ijumaa kuwa ametengana na mpenziwe Nelly Oaks yalikuwa ni utani tu.

Mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa mahusiano yake na Oaks bado yapo imara na kuwakosoa wale walioamini madai hayo.

"Watu daima wanasubiri uanguke. Hakuna anayetaka ukiwa na furaha. Wanakimbilia utani. Habari za mahusiano zinauza tu wakati yanasambaratika. Unions tukiachana leo," Akothee alisema kupitia Instagram.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42 alimhakikishia mpenzi wake kuwa hana mpango wa kutengana kwao.

"Hata wewe unajua huwezi kuniacha, utapeza kitu hicho kwa hivyo kaa hapa Nelly Oaks," Akothee alimwandikia mpenziwe.

Hapo awali Akothee alikuwa amedai kwamba yupo single tena baada ya "mpaka kifo kitakapotutenganisha" kumwacha.

"Nipo single tena wadau. Barabara ya kuelekea kwa mahusiano daima huwa katika harakati za kutengenezwa," Alisema.

Akothee na Nelly Oaks wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miaka minne. Hata hivyo hawana mtoto yeyote pamoja.