Hongera! Njugush na mkewe wanatarajia mtoto wa pili

Muhtasari

•Wanandoa hao walifichua ujauzito katika Tamasha la TTT ambalo waliandaa Ijumaa katika ukumbi wa Nairobi Cinema.

Image: INSTAGRA// BLESSED NJUGUSH

Mchekeshaji Timothy Kimani almaarufu Njugush na mke wake Celestine Ndinda wanatarajia mtoto wao wa pili.

Wanandoa hao walifichua ujauzito katika Tamasha la TTT ambalo waliandaa Ijumaa katika ukumbi wa Nairobi Cinema. Hata hivyo hawakufichua mengi kuhusu safari ya ujauzito huo.

Wawili hao ambao pia ni waigizaji wenza wamekuwa katika ndoa kwa takriban miaka sita na tayari wana mtoto mmoja wa kiume pamoja, Tugi. Walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza mwezi Machi, 2018.

Takriban miaka miwili iliyopita, Bi Ndinda alilazimika kujitokeza kuweka mambo wazi kufuatia uvumi uliokuwa umeenea kwamba ni mjamzito.

"Picha hizo ni za ujauzito wangu wa kwanza," Ndinda alijibu kufuatia picha za ujauzito zilizokuwa zinaenezwa.

Njugush na Ndinda walifunga pingu za maisha mwezi Desemba 2016 na wakagundua ujauzito wa mtoto wao wa kwanza rtakriban miezi  minne baadae.

Wawili hao waliwahi kufichua kwamba walikuwa wamekumbwa na uhaba wa fedha katika kipindi ambacho walipata mtoto wa kwanza.