Shabiki wa Harmonize achorwa tattoo ya barua ya msamaha akimsihi Kajala amrudie

Muhtasari

•Shabiki huyo amewashangaza wengi baada yake kuchorwa tattoo ya barua ya msamaha katika juhudi za kumshawishi Kajala kumrudia Harmonize.

•Shabiki huyo aliendelea kumbainishia Kajala kwamba Harmonize bado anampenda sana huku akimsihi amrudie ili wajenge familia pamoja.

Shabiki wa Harmonize achorwa tattoo ya barua ya msamaha akimsihi Kajala amrudie
Shabiki wa Harmonize achorwa tattoo ya barua ya msamaha akimsihi Kajala amrudie
Image: HISANI

Shabiki mmoja wa staa wa Bongo Harmonize amejitolea kusaidia msanii huyo kumwomba msamaha aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala Masanja.

Shabiki huyo amewashangaza wengi baada yake kuchorwa tattoo ya barua ya msamaha katika juhudi za kumshawishi Kajala kumrudia Harmonize.

"Dada yangu Kajala Masanja, wewe ndio furaha ya moyo wake. Uwepo wako kwake ni wa maana sana katika maisha yake. Naomba umsamehe Harmo, mpe nafasi nyingine moyoni mwako," Sehemu ya barua hiyo ilisoma.

Kupitia tattoo yake, shabiki huyo aliendelea kumbainishia Kajala kwamba Harmonize bado anampenda sana huku akimsihi amrudie ili wajenge familia pamoja.

"Karibu tena, bado tunakupenda sana," Tattoo hiyo ilisoma.

Katika kipindi cha takriban mwezi mmoja ambacho kimepita Harmonize amekuwa akijitahidi kumshawishi mama huyo wa binti mmoja akubali warudiane.

Konde Boy amefanya mengi makubwa katika juhudi za kumtongoza Kajala akubali ombi lake la kurudiana.

Miongoni mwa mambo ambayo mwanamuziki huyo amefanya ni pamoja na kumnunulia gari aina ya Range Rover, kuweka bango barabarani, kumnunulia mkufu wa thamani, kutundika picha yake katika chumba chake cha kulala kati ya mengine mengi.