Usimuamini pasta wako muamini Mungu-Ushauri wa Huddah kwa Wakristo

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti maarufu nchini Huddah Monroe, ametoa ushauri wa kipekee kwa mashabiki wake ambao ni wakristo
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti maarufu nchini Huddah Monroe, ametoa ushauri wa kipekee kwa mashabiki wake ambao ni wakristo.

Huddah anafahamika sana kwa semi zake mitandaoni, na pia kupitia bidii ya kazi yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, katika Insta Stories Mwanasosholaiti huyo aliwashauri mashabiki wake wawee kumuamini Mungu wala sio muhubiri wao.

Ni nyakati nyingi ambazo wakristo wengi wamekuwa wakiwaamini wahubiri mbali mbali  na kuhudhuria kanisa kwa ajili ya kutendewa miujiza.

Wengi wao uamini kwamba hawana imani ya kujiombea na kupata walichoamini na kuombea.

Huddah alikuwa anajibu ujumbe unaosoma;

'Natamani wazazi wa Afrika wangesukuma masomo ya pesa jinsi wanavyosukuma dini."

Huddah alijibu na kusema;

"Dini imemaliza waafrika, amini Mungu na wala sio pasta wako," Alisema Huddah.