"Ananipenda sana!" Mwanamitindo Miriam Odemba afunguka kuhusu uhusiano wake na Ibraah

Muhtasari

•Malkia huyo mwenye umri wa miaka 40 alifichua kuwa alikuja kujuana na Ibraah kupitia bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize.

•Odemba pia alisema hana uhasama wowote na wasanii wa WCB licha ya kuwa ana uhusiano wa karibu zaidi na wale wa Kondegang.

Ibraah na Miriam Odemba
Ibraah na Miriam Odemba
Image: INSTAGRAM// IBRAAH

Mwanamitindo mashuhuri wa Bongo Miriam Odemba amefafanua zaidi kuhusu uhusiano wake wa karibu na msanii wa Kondegang Ibrahim Abdallah Nampunga almaarufu Ibraah.

Akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Odemba alifichua kuwa Ibraah uhusiano wake na Ibraah ni wa kirafiki tu.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka 40 alifichua kuwa alikuja kujuana na Ibraah kupitia bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize.

"Kwa kweli Ibraah ni rafiki yangu. Ni kupitia Harmonize nimemjua Ibraah. Napenda sana muziki wake. Ni mdogo wangu ananiheshimu na ananipenda sana," Alisema.

Mwanamitindo huyo alieleza kuwa kwa kawaida Ibraah humchukulia kama dadake mkubwa.

"Ananipenda mimi kama dadake. Ndio maana kuna kipindi alinipa namba yake ya simu lakini nikawa simpigii simu. Kuna siku alinipigia simu nikawa nimefurahi. Nilifurahi na kusem kwa kweli mdogo wangu kanikumbuka," Alisema.

Odemba pia alisema hana uhasama wowote na wasanii wa WCB licha ya kuwa ana uhusiano wa karibu zaidi na wale wa Kondegang.

Aliweka wazi kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na  bosi wa WCB Diamond Platnumz na kufichua kuwa huwa anapata sapoti yake kubwa katika kazi zake.

"Mimi sina utimu. Kwa sababu namsapoti Harmonize haimaanishi eti simsapoti Diamond ama Zuchu. Mimi ni dada ambaye najiheshimu, ni dada ambaye napenda  vipaji," Alisema.

Odemba aliwashauri wasanii wa Tanzania kuungana na kuwaonya dhidi ya kujigawanyisha katika makundi.