Msanii Harmonize atiwa mbaroni

Muhtasari
  • Mwimbaji huyo amekuwa nchini tangu Ijumaa.Alikuwa aondoke Jumapili
  • Tangu kuwasili kwake nchini, mwimbaji huyo amekuwa na washiriki kadhaa
Image: HISANI

Mwimbaji wa Tanzania Harmonize amekamatwa, anazuiliwa katika vituo vya polisi vya Kileleshwa.

Kulingana na nduru za habari ni kuwa nyota huyo wa muziki alikamatwa kuhusiana na kashfa iliyokuwa ikiendelea ya kudaiwa kukosa kuonekana katika vilabu kadhaa jijini Nairobi licha ya kupokea pesa kwa ajili yake.

Kukamatwa kwake kulikuja saa chache baada ya kutumbuiza katika tamasha katika KICC jijini Nairobi.

Mwimbaji huyo amekuwa nchini tangu Ijumaa.Alikuwa aondoke Jumapili

Tangu kuwasili kwake nchini, mwimbaji huyo amekuwa na washiriki kadhaa.

Siku ya Ijumaa, kulikuwa na mpambano mkali kati ya Harmonize na washereheshaji katika klabu moja jijini Nairobi.

Eric Omondi ambaye alikuwa na msanii huyo alisema kuwa kulikuwa na kutoelewana kutoka kwa mashabiki kuhusu kile ambacho Harmonize alitarajiwa kufanya katika klabu hiyo.

"Mambo mengi yalitokea, ilikuwa sherehe na baadhi ya watu walisisimka... klabu ilikuwa ndogo. Kuna tofauti kati ya tamasha na/au tukio. Wakenya lazima waelewe kwamba ilikuwa ni mwonekano wa klabu/mwonekano wa kiufundi/kukutana na kusalimiana/ tafrija ya ziada,” Eric Omondi alisema.