Mwanangu hakukataa kumsalimia Raila Odinga-Jimmy Kibaki azungumza

Muhtasari
  • Ni video ambayo ilizua mjadala mkali mitandaoni huku, wakenya tofauti wakitoa hisia tofauti kuhusiana na video hiyo
Jimmy Kibaki
Image: EZEKIEL AMING'A

Huku mazishi ya hayati Mwai KIbaki yakiendelea siku ya Jumamosi, viongozi mbalimbali walijitokeza na kuomboleza pamoja na familia ya rais huyo mstaafu.

Kupitia kwenye mitanao ya kijamii video ya kinara wa ODM Raila Odinga akimsalimia mjukuu wa Mwai na kisha akakataa ilienea.

Ni video ambayo ilizua mjadala mkali mitandaoni huku, wakenya tofauti wakitoa hisia tofauti kuhusiana na video hiyo.

Walioshiriki walidai mjukuu alikataa kumsalimia kiongozi wa ODM.

Fact-checker hata hivyo imethibitisha kuwa video imehaririwa kwa nia ambayo bado haijajulikana.

Mdadisi huyo amegundua kuwa mjukuu huyo alimsalimia waziri mkuu huyo wa zamani na ni baada ya kumsalimia ndipo alipompa mgongo.

Huku Jimmy KIbaki akizungumzia suala hilo, kupitia kwenye ukurasa wake rasmia ya twitter amesema kwamba mwanawe hakukataa kumsalimia kinara huyo.

Zaidi ya yote amewauliza wakenya kuelewa kuhusu hisia za mtu,na kwamba familia yao inapitia wakati mgumu.

"Hakuna anayeweza kudhibiti hisia. Mwanangu hakukataa kumkumbatia Rt mheshimiwa Raila Odinga. Sisi kama familia tunakabiliwa na nyakati ngumu. Kuelewa hisia," JImmy Alisema.