Lengo langu kuu si kuwa maarufu bali tajiri-Msanii Jovial afichua haya

Muhtasari
  • Msanii huyo pia amefichua kwamba anaogopa umaskini, na kwamba alifanya maamuzi mabaya awali katika maisha yake
Jovial KE
Image: Facebook

Msanii maarufu Jovial anafahamika sana kwa ajili ya sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni, na bidii yake katika kazi yake ya usanii.

Kupitia kwenye insta stories msanii huyo amefichua kwamba kuna wakati alikuwa anafanya maamuzi kutokana na hisia zake huku akisema kwamba mambo mengi yalimpitia kwa ajili ya tabia zake.

Msanii huyo pia amefichua kwamba anaogopa umaskini, na kwamba alifanya maamuzi mabaya awali katika maisha yake.

"Kuna wakati ambao nilikuwa nafikiria na hisia na kabla ya kufanya maamuzi ningeshikwa na hisia hata mahali pasipo stahili hisia

Nafasi zikawa zinaniponyoka maskini Jovial kwa sababu ya kufanya maamuzi mabaya, unaweza sema una maadui kumbe adui yako ni wewe mwenyewe," Alisema Jovial.

Msanii huyo aliweka wazi kwamba lengo lake kuu ni kuwa tajiri na wala sio maarufu.

"Nikaja nikaona nitakufa maskini, na ninavyoogopa shida mimi, ukwei ni kuwa lengo langu kuu ni sikuwa maarufu bali kuwa tajiri, Mungu wangu nahitaji kuwa tajiri, epuka kufanya maamuzi mabaya kutokana na hisia."