"Babangu ni mzuri!" Paula Kajala amtambua na kumsifia baba yake mzazi

Muhtasari

•Paula alitumia ukurasa wake wa Instagram kumtambua mzazi huyo wake huku akiisifia sana sura yake.

•P-Funk na mwigizaji Fridah Kajala Masanja walikuwa kwenye mahusiano kwa muda ila yakagonga mwamba

Paula Kajala, P-Funk Majani
Paula Kajala, P-Funk Majani
Image: INSTAGRAM

Mwanamitindo Paula Paul Majani amemsherehekea baba yake mzazi Paul Matthysse almaarufu P-Funk Majani.

Paula alitumia ukurasa wake wa Instagram kumtambua mzazi huyo wake huku akiisifia sana sura yake.

"Nyie nyie nyie, Baba yangu ana sura nzuri. Baba yangu wa pekee," Paula aliandika chini ya picha ya P-Funk.

Katika mahojiano ya hapo awali, P-Funk aliwahi kudai kuwa Paula aliwahi kumkana kuwa baba yake mzazi.

"Tayari nimenawa mikono yangu. Mtoto huyo anatafuta laana. Aliwahi kuniambia kuwa mimi sio baba yake. Kajala sio familia yangu," P-Funk alisema kuhusiana na drama zilizofuatia kuvunjika kwa mahusiano ya Kajala na Harmonize. 

Hata hivyo, kwa sasa hayo yanaonekana kuwa ndani ya kaburi la sahaukwa kuwa hata sio mara ya kwanza kwa Paula kumtambua  hadharani mtayarishaji huyo kama babake.

Image: INSTAGRAM// PAULA KAJALA

P-Funk ni mtayarishaji wa muziki na pia ni mmiliki wa Studio za Bongo Records. Ana uzoefu mkubwa katika mzuki aina ya Bongo na Hiphop.

Miaka mingi iliyopita, P-Funk na mwigizaji Fridah Kajala Masanja walikuwa kwenye mahusiano kwa muda ila yakagonga mwamba. Katika kipindi cha mahusiano yao, Kajala alipata ujauzito na kujifungua Paula takriban miongo miwili iliyopita.

Baada yao kutengana, P-Funk alifunga ndoa na mwanamke mwingine anayefahamika kama Samira. Kwa upande wake Kajala amefanya majaribio kadhaa ya mahusiano ikiwemo na Harmonize ila hayajaweza kudumu.

Katika kipindi cha mwezi mmoja ambacho kimepita Harmonize amekuwa akijaribu kuomba msamaha na kurejesha mahusiano yake na Kajala. Ilidaiwa kuwa wawili hao walitofautiana baada ya Harmonize kujaribu kumtongoza Paula.