"Juju haikukaa sana kwangu!" Aliyekuwa mpenzi wa Amber Ray amshtumu kwa kutumia uchawi

Muhtasari

•IB Kabba amemshtumu mama huyo wa mtoto mmoja kwa kumfanyia uchawi wakati wa mahusiano yao ya muda mfupi.

•Kabba  amewasihi wanaume kuwa makini zaidi na wanawake wanaochumbiana nao huku akidai kuwa baadhi yao ni hatari.

Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wake IB Kabba
Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wake IB Kabba
Image: HISANI

Mchezaji mpira wa vikapu kutoka Sierra Leone IB Kabba amethibitisha kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na mwanasoshalaiti Amber Ray.

Amber Ray alimtambulisha mwanariadha huyo kwa wanamitandao mwezi Februari ila baada ya kipindi kifupi mahusiano yao yakagonga mwamba.

IB Kabba sasa anamshtumu mama huyo wa mtoto mmoja kwa kumfanyia uchawi wakati wa mahusiano yao ya muda mfupi.

"Mimi ni mtu huru kama Mandela. Juju haikukaa sana kwangu. Asante Mungu kwa kunisaidia," IB Kabba amesema kupitia Instagram.

Hapo awali IB Kabba alikuwa amedokeza kuwa mahusiano yake ya kipindi kifupi na Amber Ray yalikuwa 'sumu.'

"Amepindishwa kila kitu, kwanini nitake kudhibiti maisha yake? Alikuwa akitumia simu yangu na ku-block watu kwenye Instagram na sijawahi kuingia kwenye simu yake. Nilichokuwa najaribu kujenga na alichokuwa anajaribu kukifanya, Ujenzi ulikuwa tofauti. Haikufaulu." Kabba alisema kwenye mahojiano.

Kabba  amewasihi wanaume kuwa makini zaidi na wanawake wanaochumbiana nao huku akidai kuwa baadhi yao ni hatari.

"Tuwe makini na baadhi ya wanawake ambao watakuja katika maisha yetu, simdharau mwanamke yeyote, ninawaheshimu wanawake na nitawapenda milele lakini daima tuwe makini na kupata wanaofaa. Mungu akubariki," Kabba aliandika kwenye Instastori zake.

Hivi majuzi Amber Ray aliweka wazi kuwa yupo single baada ya kutengana na IB Kabba.