Najililia mwenyewe-Aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy akiri kupambana na msongo wa mawazo

Muhtasari
  • Aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy akiri kupambana na msongo wa mawazo

Aliyekuwa mpenzi wa Stivo Simple Boy , Pritty Vishy ametumia ukurasa wake wa Instagram kukiri kwamba anapambana na msongo wa mawazo.

Anasema kuwa kupambana na unyogovu ndio jambo gumu zaidi kufanya kwani watu wanaweza kufikiria kuwa uko sawa kwa sababu unatabasamu nao lakini unalia peke yako.

Pritty Vishy na mwimbaji Stivo walikomesha uhusiano wao ambao sio wa muda mrefu sana miezi michache iliyopita.

Pritty alionekana kufanya vyema kulingana na picha zake za Instagram na hata alifanikiwa kupata kazi ya ubalozi.

"Kujaribu kupambana na unyogovu ๐Ÿ˜ชndilo jambo gumu zaidi hili... inabidi uonekane sawa wakati hauko sawa..lazima utabasamu ukiwa nao..kitu pekee ninachofikiria kufanya vizuri zaidi ni kulia peke yangu na kulia. tabasamu nao kama ila kitu kiko sawa lakini hakiko sawa๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”," Pritty Amekiri.

Mashabiki walitumia fursa hiyo kumfariji Pritty.

Awali akiwa kwenye mahojiano, mwanadaa huyo alisema na kukiri kwamb akiwa kwenye uhusiano na msanii huyo alimcheza na wanaume wengine.