Mkewe Njugush afunguka kuhusu ujauzito wake na sababu ya kuchagua CS wakati wa kujifungua

Muhtasari
  • Mkewe Njugush afunguka kuhusu ujauzito wake na sababu ya kuchagua CS wakati wa kujifungua
Image: INSTAGRAM// CELESTINE NDINDA

Celestine Ndinda ni mmoja wa waigizaji maarufu nchini Kenya na kwa sasa anafanya maudhui ya kustaajabisha na mumewe Njugush.

Akiwa kwenye mahojiano, Celestine Ndinda alifunguka mambo ambayo amekuwa akipitia wakati bado ana ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Aliendelea kwa kusema kuwa anapokea shutuma kutoka kwa mashabiki wake na hili ni jambo ambalo anakumbana nalo kwa sasa katika safari yake ya ujauzito.

Aliendelea kusimulia uzoefu wake wa wakati mgumu kutoka kwa shabiki wake ambaye alimuuliza kuwa ikiwa ni mjamzito au amebeba tembo na jambo hili halisi lilimfanya ahisi huzuni na kutoheshimiwa.

Zaidi ya hayo, aliwasihi mashabiki wake watulie na siku atakapojifungua atashiriki nao habari njema lakini kwa sasa wanaacha kusema mambo hasi kuhusu ujauzito wake.

Pia alisema kwa sasa anaelewa uchungu wake wa uzazi na ataenda thieta mapema ili aweze kuzuia maumivu zaidi aliyoyapata katika ujauzito wake wa kwanza.

 ”Jambo moja ambalo nina uhakika nalo wakati huu, sitahisi maumivu. Ninataka tu kwenda moja kwa moja kwenye thieta. Hio by the way nimewaambia juu ya kwanza I felt so much pain… Hii nimejiambia sichoki. Hilo ndilo jambo pekee ninalojua," Alisema Celestine.