Show tano ambazo unapaswa kutazama kwenye showmax kwa sasa

Nyota wa show hiyo ni Sarah Hassan anaigiza kama afisa wa upelelezi Makena na Alfred Munyua anayeigiza kama afisa wa upelelezi Silas.

Muhtasari
  • Je, unajua unaweza tazama vipindi vyote vya msimu wa pili uliotarajiwa sana wa mchezo wa kuigiza nchini Kenya wa Crime and Justice?
  • Single Kiasi inafuata marafiki watatu mjini Nairobi - Sintamei, Mariah na Rebecca - wanaposhughulikia ndoa, uhusiano, na kazi. 
Image: Showmax

Kama unatafuta maonyesho ya kutizama wikendi inayojiri ama jioni baada ya kazi, tuko na show tano ambazo unapaswa kutizama kwa sasa kwenye Showmax.

  1. Crime and Justice Season 2

Je, unajua unaweza tazama vipindi vyote vya msimu wa pili uliotarajiwa sana wa mchezo wa kuigiza nchini Kenya wa Crime and Justice?  Wanaoigiza kwenye kipindi hicho ambacho ni cha kwanza cha Showmax Original nchini ni nyota Sarah Hassan ambaye anaigiza kama afisa wa upelelezi Makena na Alfred Munyua ambaye anaigiza kama afisa wa upelelezi Silas.

Season 2 itachunguza maisha ya kibinafsi ya Makena na Silas, hata wakati wanaendelea kuchunguza uhalifu jijini Nairobi. Pia itaangalia zaidi mfumo wa haki, na nguvu zinazoidhibiti.

Crime and Justice season 2 pia inatambulisha baadhi ya sura mpya, ikiwa ni pamoja na Mumbi Maina (The Matrix Resurrections, Sense8), Charles Ouda (Makutano Junction, The First Grader) na Sheila Munyiva (Rafiki, Country Queen).

2. Eno

Eno ndio kipindi cha kwanza cha Showmax Original nchini Ghana. Tamthilia hii inafuata Abena Baafi, mama mmoja ambaye amedhamiria kuingilia maisha ya binti zake watatu kwa kuwaongoza kuelekea kwenye njia ya wachumba matajiri. Mama anaweza kujua vizuri zaidi lakini binti zake wangependelea kufuata njia yao wenyewe.

3. Single Kiasi

Single Kiasi inafuata marafiki watatu mjini Nairobi - Sintamei, Mariah na Rebecca - wanaposhughulikia ndoa, uhusiano, na kazi. 

4. The Real Housewives of Lagos

 Tazama The Real Housewives of Lagos kwenye Showmax kila Ijumaa. Kwa mtindo wa kweli wa Lagos, watakuwa wakionyesha mitindo yote ya juu ya fashion, anasa na pesa.

Nyota wa #RHOLagos ni Carolyna Hutchings, Laura Ikeji, Chioma Ikokwu, Toyin Lawani-Adebayo, Iyabo Ojo and Mariam Timmer.

5. Ziwe

Mfululizo wa kuchekesha, aina mpya unaomshirikisha mwandishi, mchekeshaji na internet sensation Ziwe. Kipindi chake ni mchanganyiko wa muziki, mahojiano na michoro ambayo inapinga kanuni za Amerika.