Simpendi yeye sio aina yangu-Msanii Stivo Simple Boy asema kuhusu aliyekuwa mpenzi wake Vishy

Muhtasari
  • Akiwa kwenye mahojiano na Mwimbaji The-Star alisema  kwamba havutiwi naye tena
Image: INSTAGRAM// STIVO SIMPLE BOY

Stivo Simple Boy amemuonya aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy. Kulingana na Stivo mwanadada huyo anapaswa kuhesabu hasara zake na kuendelea kwani yeye si wa aina yake.

Akiwa kwenye mahojiano na Mwimbaji The-Star alisema  kwamba havutiwi naye tena.

“Sivutiwi naye tena. Tuliachana kwa sababu ya tabia yake mbaya. Hakuwa mwaminifu na alikuwa na mtazamo. Yeye sio aina yangu tena."

Simple Boy aliongeza kuwa anatafuta mwanamke ambaye ana tabia nzuri.

“Sitafuti urembo wala kujipodoa. Niko tayari kutulia lakini na mtu sahihi.”

Stevo alikuwa akichumbiana na Pritty lakini waliachana siku chache baada ya kuonekana na mwimbaji wa Mombasa, Adasa.

Sasa anasema hakukuwa na chochote cha kimapenzi kilichokuwa kikiendelea kati yake na Adasa, yote yalikuwa biashara.

“Nahitaji kuliweka hili wazi. Mimi si simchumbii na sijawahi mchumbia Adasa. Tulikuwa tukifanyia kazi kolabo.”

Aliendelea kumshauri ex wake kuacha kuwinda. Lakini kwa nini waliachana?

"Ningemwambia kitu na angefanya kinyume. nilichoka.”

Hata hivyo alifichua kuwa yeye ndiye aliyemuacha.

“Simpendi. Simmiss,” alisema

Hivi majuzi Pritty alisema atahitaji milioni mbili kama mahari kwa yeyote aliye tayari kumuoa.

Huku msanii huyo akizungumzia hayo alisema kwamba;

“Ni mwanaume gani mwenye pesa za namna hiyo? Anaweza kuwa nayo lakini mwanamke anahukumiwa kwa tabia yake. Tusiangalie pesa bali tuangalie mapenzi. Ninaweza kumjua mwanamke anayependa pesa kwa kumtazama tu.”