Wafahamu wasanii wa Afrika wanaomiliki ndege za kibinafsi

Muhtasari

•Diamond alitangaza mpango wake siku wa Jumatano wakati alipokuwa anamtakia meneja wake El-Jefe Mendez heri za siku ya kuzaliwa.

•Familia ya Cuppy inaripotiwa kumiliki ndege ya kibanfsi ambayo msanii huyo hutumia katika ziara zake.

Diamond Platnumz, DJ Cuppy, Davido
Diamond Platnumz, DJ Cuppy, Davido
Image: HISANI

Ni rasmi kwamba nyota wa Bongo Diamond Platnumz anatazamia kununua ndege kufikia mwisho wa mwaka huu. 

Diamond alitangaza mpango wake siku wa Jumatano wakati alipokuwa anamtakia meneja wake El-Jefe Mendez heri za siku ya kuzaliwa.

"Tulinunua 2021 Rolls Royce Black Bedge Zero Kilometre mwaka jana, na tunanunua ndege ya kibinafsi mwaka huu!! hiyo ndio tafsiri ya kuwa na usimamizi bora!! Ni Siku ya Kuzaliwa ya meneja wangu Sallam Sk," Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Bosi huyo wa WCB hata hivyo hatakuwa msanii wa kwanza barani Afrika kumiliki ndege ya kibinafsi.

Kuna baadhi ya wasanii na watu mashuhuri hasa kutoka Afrika Magharibi ambao wamewahi kununua ndege za usafiri wao wa kibinafsi.

1. Davido

Image: HISANI

Mwanamuziki wa Afropop David Adedeji Adeleke almaarufu Davido anaripotiwa kumiliki ndege aina ya Bombardier Global Express 6000.

Raia huyo wa Nigeria alinunua ndege hiyo inayodaiwa kugharimu mabilioni ya pesa miaka michache iliyopita.

2. Wizkid

Wizkid ni msanii mwingine wa Afropop kutoka Nigeria anayeripotiwa kuwa mmiliki wa ndege ya kibinafsi.

3. DJ Cuppy

Image: HISANI

Mchezasanturi wa Florence Ifeoluwa Otedola almaarufu DJ Cuppy ni msanii ambaye amebahatika kuzaliwa katika familia ya kitajiri.

Familia ya Cuppy inaripotiwa kumiliki ndege ya kibanfsi ambayo msanii huyo hutumia katika ziara zake.

4. Don Jazzy

Mzalishaji mashuhuri Don Jazzy pia anaaminika kuwa miongoni mwa wasanii wa Nigeria wanaomiliki ndege za kibinafsi.

Jazzy anapendelea kufanya ziara zake za kimataifa kutumia ndege ya kibinafsi.