Naweza penda mtu mwingine aje nikiota nawe kila usiku?Harmonize amuuliza Kajala

Muhtasari
  • Hivi majuzi tumemuona staa huyo akimununulia Kajala gari kadhaa na zawadi ili aweze kumkubali tena
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa bongo angali bado mitandaoni huku akimuomba aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala msamaha huku akimtaka amrudie.

Hivi majuzi tumemuona staa huyo akimununulia Kajala gari kadhaa na zawadi ili aweze kumkubali tena.

Harmonize alionyesha magari hayo mawili kupitia mtandao wa Instagram na kumsihi mwigizaji huyo akubali kumsahe na warejeshe mahusiano yao.

"Nahisi kama kwamba  unahitaji kila nilicho nacho. Kila ninachomiliki, kwa asilimia fulani nahisi  unamiliki pia. Nakupenda sana na nakupenda sana. Naomba urudi nyumbani, tuishi maisha yetu kama zamani na Mwenyezi Mungu atatubariki tupate riziki zaidi ya tunayopata sasa hivi. Najuta sana. Pole kwako, pole kwa familia na pole kwa kila mtu. Tafadhali rudi, nakupeza sana," Harmonize alisema katika video aliyopakia Instagram.

Baada ya kutangaza kuwasili kwa magari hayo, Harmonize ameonekana akiyatumia kusafiri katika maeneo mbalimbali. Harmonize amepakia video kadhaa zikionyesha akiwa ndani ya magari hayo akienda na kutoka kufanya mazoezi katika Gym.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Jumatano msanii huyo amemuuliza mwigizaji huyo anaweza aje kumpenda mwanamke mwingine ilhali amekuwa akiota naye kila usiku.

"Naweza mpenda mtu mwingine aje wakati kila usiku naota nawe,kila mtu kutana na mtu ambaye naenda kufa naye," Aliandika Harmonize.