Afueni kwa Harmonize baada ya Kajala kum-unblock kwenye Instagram

Muhtasari

•Ni rasmi kuwa Kajala amepiga hatua ya kuondoa kizuizi ambacho alikuwa amewekea Harmonize kufuatia kutengana kwao.

•Haya yanajiri takriban mwezi moja unusu baada ya Harmonize kutoa ombi kwa muigizaji huyo kuacha kumfungia kwenye Instagram

Harmonize na Kajala Masanja
Harmonize na Kajala Masanja
Image: HISANI

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali sasa anaweza kutabasamu baada ya mpenzi wake wa zamani Frida Kajala Masanja kum-unblock kwenye Instagram.

Ni rasmi kuwa mama huyo wa binti mmoja amepiga hatua ya kuondoa kizuizi ambacho alikuwa amewekea Harmonize kufuatia kutengana kwao.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE TZ

Akaunti ya Kajala sasa inaweza kuonekana miongoni mwa watu Konde Boy anafuata kwenye Insagram. Hiyo ina maana kuwa Harmonize sasa anaweza kufuatilia chapisho zote za mpenzi huyo wake wa zamani na hata kuchapisha maoni yake chini yake.

Kajala mwenyewe hata hivyo hamfuatilii Harmonize kwenye Instagram labda kwa sababu zake binafsi.

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Haya yanajiri takriban mwezi moja unusu baada ya Harmonize kutoa ombi kwa muigizaji huyo kuacha kumfungia kwenye Instagram

Harmonize alitoa ombi hilo mapema mwezi Aprili baada ya kumnunulia muigizaji huyo mkufu wa dhahabu kwa Tsh. 5M

"Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu ambaye unapenda sana. Wa kupeleka sasa!! Milioni 5 kwa pambo la dhahabu.," Harmonize aliandika kwenye Instastori.

Aliongeza,"Mtu mmoja tafadhali amwambie anifungulie kwenye Instragram."

Licha ya juhudi zote ambazo Harmonize alifanya kuonyesha mkufu huo ghali kwenye ukurasa wake wa Instagram, Kajala hakuweza kuona moja kwa moja kwa kuwa tayari alikuwa amemblock msanii huyo.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidai kwamba aliamua kununua mkufu huo kwa sababu anafahamu fika kuwa Kajala anapenda dhahabu.

“Anapenda Mungu na Dhahabu. Hii ni hatari, jamani mtu amwambie akubali kunirudia. Ni jambo la kimboleambolea kutumia pesa zako kwa mtu unayempenda. Tafadhali mtu amwambie aniondoe kwenye listi ya block, Instagram,” Harmonize alisema.

Katika kipindi cha mwezi mmoja ambacho kimepita mwanamuziki huyo amekuwa akiandika jumbe nyingi za msamaha kwenye Instagram ila mwenye kuandikiwa hajakuwa akizisoma moja kwa moja. 

Ni afueni kubwa sasa kwa Harmonize kwa kuwa mpenzi huyo wake wa zamani huenda sasa atakuwa anaziona chapisho zake zote.

Hatua hiyo pia inamaanisha kuwa mwanamuziki huyo anaweza kumtumia Kajala jumbe kupitia Instagram na akaweza kuzipokea na kujibu.