Mwigizaji Omosh azungumza baada ya kuombewa na Pastor Kanyari

Muhtasari
  • Mwigizaji Omosh azungumza baada ya kuombewa na Pastor Kanyari
Image: INSTAGRAM// OMOSH KIZANGILA MWENYEWE

Mwigizaji Joseph Kinuthia almaarufu Omosh amekuwa gumzo tena mitandaoni baada ya video yake akianguka wakati akiombewa na mhubiri mashuhuri Victor Kanyari kusambaa.

Katika video hiyo Omosh anaanza kwa kujitambulisha kisha anaendelea kueleza jinsi alivyojipata katika kanisa la Kanyari.

Mwigizaji huyo wa Tahidi High alieleza kuwa aliamua kupiga hatua hiyo baada ya rafiki yake kumshawishi ahudhurie ibada ya kanisa. Baada ya ibada ndipo Kanyari alimpatia msanii huyo nafasi ya kutoa ushuhuda wake.

"Leo nimesoma kuhusu madhabahu. Nikiwa nimekaa pale chini nimeona labda mambo yangu huenda mrama kwa kuwa sijajenga madhabahu vizuri. Hapa nimesoma lazima nijenge madhabahu yangu ili naye Mungu ashuke anene nami," Omosh alisema mbele ya waumini waliokuwa wamejumuika pale kanisani.

Omosh alisema yupo tayari kutengeneza madhabahu yake na Mungu vizuri baada ya kusikiliza mahuburi ya Kanyari.

Huku akizungumzia video hiyo ambayo imeenea sana mitandaoni alisema kuwa;

"I'm on a rooftop, I'm high and I am with the most high and I have the spirit, but not Konyagi. Try God so you can feel the high I feel. Ah maisha  joh tukicheki mazee niko rooftop niko place high yani na niko place high na niko na the most high na niko na spirit na sio ya konyagi, try him, try God usikie vile nasikia niko high na most high au sio?"