logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa nauza matumbo ili kujikimu-Amber Ray afunguka kuhusu maisha yake

Alisema kuwa maisha hayakuwa rahisi hata kidogo baada ya wazazi wake kujua kwamba alikuwa mjamzito.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 May 2022 - 11:16

Muhtasari


  • Alisema kuwa maisha hayakuwa rahisi hata kidogo baada ya wazazi wake kujua kwamba alikuwa mjamzito

Faith Makau almaarufu Amberay leo ameshiriki hadithi yake chungu kuhusu mafanikio yake.

Wakati wa mahojiano na mcheshi Oga Obinna ambaye aliandaa Amberay kwa mahojiano ya kushangaza.

Amberay alisema kuwa maisha yake yalibadilika kabisa baada ya kupata ujauzito akiwa bado mdogo.

Alisema kuwa maisha hayakuwa rahisi hata kidogo baada ya wazazi wake kujua kwamba alikuwa mjamzito.

Alisema kitu pekee ambacho mama yake na baba yake walimwambia ni kwamba watamsaidia kumlea mtoto huyo.

Aliendelea na kusema baada ya kujifungua mtoto wa kiume wazazi wake hawakujishughulisha kumsaidia vitu ambavyo mtoto huyo alivihitaji hivyo ikamlazimu kuanza na kuuza "Matumbo" ili apate mtaji.

"Sijawahi enda chuo kikuu wala kwenye taasisi yeyote, nilisoma katika shule tatu za sekondari, baada ya muda baba yangu alipoteza kazi yake kwa hivyo familia yangu ikawa na shida ya pesa, mimi ndite kifungua mimba

Kuna wakati nilikosa mpaka baba yangu alikuwa karibu kunipeleka jela, baba yangu alikuwa polisi,mama yangu hakusema chochote kwani baba alikuwa mkali sana

Nilianza kuuza maziwa lakini kwa kuwa sipendi kuamka mapema, nikabadilisha biashara na nikaanza kuuza matumbo ili niweze kujikimu," Alieleza Amber Ray.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved