'Huwa natumia bangi kumaliza Depression,'Msanii wa Gengetone afichua

Muhtasari
  • Zzero alisema bangi imekuwa na jukumu kubwa sana katika kumsaidia kupambana na msongo wa mawazo
ZZERO SUFURI

Hitmaker wa Zimenishika na mmoja wa msanii maarufu wa Gengetone kutoka Kenya Zzero Sufuri, amezua taharuki tena mtandaoni baada ya kufichua jinsi anavyokabiliana na msongo wa mawazo.

Zzero alisema ni kweli kuna baadhi ya wasanii wa Gengetone wamekata tamaa kutokana na muziki wao kuporomoka.

Hata hivyo yeye mwenyewe hajawahi kuwa na msongo wa mawazo kwa sababu kila anapojisikia chini sana au mambo yanakaribia kwenda kushoto, ananunua bangi na kuanza kuivuta.

Zzero alisema bangi imekuwa na jukumu kubwa sana katika kumsaidia kupambana na msongo wa mawazo.

Alisema yeye huwa na furaha na hali ya juu hivyo kumpata upande mbaya ni nadra sana.

Zzero alisema kuwa atamuunga mkono Wajackoya na anatamani sana ashinde uchaguzi wa urais kwa sababu atahalalisha bangi na hii itasaidia baadhi ya watu kupambana na msongo wa mawazo vizuri sana.

Zzero alisema kuwa amekuwa kimya kwa muda kwa sababu amekuwa akifanyia kazi albamu yake ambayo itatoka hivi karibuni.

"NIlikuwa niachie albamu yangu mwezi wa sita lakini niliahirisha,kwa sababu ya jambo moja au lingine lakini wasanii wanapaswa kutarajia jambo nzuri na miziki nzuri kutoka kwa albamu yangu

Sijawahii patwa na msongo wa mawazo kwani nikiskia hivo huwa natumia bangi, naskia vyema sio kula vitu ambavyo havieleweki ndio zinafanya huwe na drepression."