Rick Ross azungumzia ziara yake ya Tanzania kupanda Kilimanjaro, kujivinjari na Hamisa Mobetto

Muhtasari

•Rick Ross ambaye ni mzaliwa wa Marekani pia alidokeza mpango wa kujenga nyumba nchini Tanzania. 

•Rick Ross alisema anatazamia sana kufika Tanzania ili aweze kuyafurahia mazingira ya nchi hiyo jirani na pia kuonana na Mobetto.

Rick Ross na Hamisa Mobetto
Rick Ross na Hamisa Mobetto
Image: HISANI

Rapa William Leonard Roberts almaarufu Rick Ross amethibitisha kuwa anapanga kuzuru Tanzania hivi karibuni.

Akiwa kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Hamisa Mobetto kwenye Instagram, Rick Ross alisema anapanga kuukwea Mlima Kilimanjaro.

"Napanga kupanda juu ya Mlima Kilimanjaro, je utakuja nami? Lazima tupande nawe juu ya Mlima Kilimanjaro," Rick Ross alimwambia Mobetto.

Mobetto alionyesha dalili za wasiwasi kuhusiana na mpango huo ila hatimaye akakubali kuandamana na rapa huyo kupanda juu ya mlima huo.

"Sitakubali upande mlima pekee yako. Nitakuwa hapo nawe," Mobetto alimjibu Rick Ross.

Rick Ross ambaye ni mzaliwa wa Marekani pia alidokeza mpango wa kujenga nyumba nchini Tanzania. 

Mobetto aliunga mkono mpango huo huku akipendekezea rapa huyo anunue kiwanja kando na bahari.

"Unafaa kununua nyumba huku. Kuna ardhi nzuri hapa.Unaweza kununua nyumba kando na bahari. Bahari ni nzuri sana. Inakaa vizuri. Kusema kweli inakaa vizuri kuliko Miami," Alisema.

Mpenzi huyo wa zamani pia alitoa pendekezo kwa Rick Ross apige hatua ya kuwekeza katika nchi yake ya Tanzania.

Rick Ross alisema anatazamia sana kufika Tanzania ili aweze kuyafurahia mazingira ya nchi hiyo jirani na pia kuonana na malkia huyo wa muziki ambaye alitambulisha kama mpenzi wake.

"Nataka kufurahia ardhi huko na kufurahia muda wangu huko pamoja na wewe," Rick Ross alisema.

Hamisa alifichua kuwa atakuwa anaenda katika jiji la Los Angeles, nchini Marekani mwezi Julai mwake huu.

Rick Ross aliahidi kuhakikisha kuwa wamepatana katika ziara hiyo,