"Nilipitia mengi" Msanii Jovial afunguka kuhusu kukumbwa na msongo wa mawazo

Muhtasari

•Jovial amefichua kuwa alikumbwa na msongo wa mawazo mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

•Amewashauri watu kushirikisha wapenzi wao kwenye mambo wanayokumbana nayo maishani ili kutafuta suluhu ya haraka.

Image: INSTAGRAM// JOVIAL

Malkia wa muziki Juliet Miriam almaarufu Jovial amefichua kuwa alikumbwa na msongo wa mawazo miezi michache iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Jovial ameeleza kuwa alipitia mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

Jovial hata hivo amebainisha kuwa sio watu wengi walifahamu kuhusu yale ambayo alikuwa anapitia kwa kuwa alificha hisia zake halisi kutoka kwa mitandao ya kijamii.

Nilikuwa na huzuni, kuharibika na kupoteza kabisa lakini hakuna mtu alijua kuhusu hilo! Kwenye mitandao ya kijamii kila mtu anafuraha, ndivyo tunavyotakiwa kuonyesha lakini ndani yetu tunakufa polepole," Jovial aliandika kwenye Instastori zake.

Mwanamuziki huyo kutoka Pwani ametumia hali yake kufahamisha watu kuhusu msongo wa mawazo.

Amewapa matumaini watu ambao wanakabiliwa na hali kama hiyo kwa sasa na kuwahakikishia kuwa kila hali huja kupita kadri siku zinavyosonga.

"Hata upitie changamoto ya aina gani itapita tu! Natumai nitaweza kusaidia mtu mahali. Shikilia hapo kesho ni siku mpya mpenzi na mwangaza," Alisema.

Jovial amefichua kuwa huwa anapenda kufunga kuhusu mambo anayokumbana nayo ili aweze ili aweze kukutana na watu wanaopitia hali zinazofanana.

Amewashauri watu kushirikisha wapenzi wao kwenye mambo wanayokumbana nayo maishani ili kutafuta suluhu ya haraka.