'Nakiri nilimkosea Diamond Platnumz,'Rafikiye Harmonize amuomba Diamond msamaha

Muhtasari
  • Rafikiye Harmonize amuomba Diamond msamaha
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Rafiki mkubwa wa Harmonize na mmoja wa watu ambao wamekuwa wakishirikiana na Harmonize kumchana Diamond Platinumz mtandaoni Hbaba hatimaye amejitokeza wazi na kumuomba Diamond Platinumz amsamehe kwa mabaya yote na mambo aliyomfanyia.

Hbaba walikuwa miongoni mwa marafiki wa karibu wa Harmonize ambao walikuwa wakisema ni kweli Diamond Platinumz anatumia nguvu za giza, alienda hadi kushambulia maisha ya kibinafsi ya Diamond na kudai kuwa hana uwezo wa kununua Rolls Royce asilia.

Baada ya kuachana na Harmonize, Hbaba amegundua makosa yake na amejishusha na kuomba msamaha kwa Diamond Platinumz na wafanyakazi wote wa Wasafi.

"Binadamu tujifunze kuomba msamaha kwa mtu uliemkosea, Nakili mbele yenu nilimkosea saaana @diamondplatnumz Narudia Nisamehe @diamondplatnumz, Ukweli nimeujua wee ni mtu wa watu kweli kweli @diamondplatnumz Unaroho yakipekee saaana sijawai ona kwakweli wee ni PEPONI moja kwa moja, kumsamehee @h.baba_ PEPONI moja kwa moja @sallam_sk @babutale @mkubwafellatmk (PEPONI MOJA KWA MOJA) MASHABIKI WA WASAFI MNISAMEHE... WASAFI CHAMA LANGU," Alliandika Hbaba.