'Alikuwa akiwaambia ni mjane,'Mwanamke asimulia jinsi mumewe alimcheza

Muhtasari
  • Uaminifu ni jambo muhimu katika maisha ya ndoa au ya uhusiano wa kimapenzi kwa kila mwanadamu
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Uaminifu ni jambo muhimu katika maisha ya ndoa au ya uhusiano wa kimapenzi kwa kila mwanadamu.

Ila kuna wale hujipata wanawaamini wenzi wao sana kuliko vile wenzi wao wanavyowaamini kisha kuishia kuwasaliti, huku wakitafuta mipango ya kando.

Asilimia kubwa ya wanandoa katika karne hii ya sasa  wamepena talaka kutokana na makosa ya nipango ya kando.

Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na mwanamke mmoja abaye alikuwa amejawa na majonzi, ya jinsi mumewe amekuwa akimcheza ilhali yeye hana hata mpango wa kando aua hana nia ya kuwa naye kwani alikuwa amaemwamini mumewe sana.

Huu hapa usimulizi wake;

"Kama kuna mwanamke ameyaona yote hii duniani ni mimi, huyu mwanamume ambaye ni mume wangu nilimwinua kutoka chini mpaka akapata kazi

Baada ya miaka 2 alianza kubadllika, na kuja nyumbani kuchelewa kummuuliza anakuwa mkali sana, nilifanya uchunguzi na nikagundua amekuwa na wanawake tofauti maishani mwaka hata kabla ya kunioa

Hata baada ya kunioa hakubadili tabia yake kwani alizidii kuwa na wanawake wengi, amekuwwa akiwadanganya kwamba yeye ni mjane mke wake aliaga dunia, sio mwanamke mmoja au wawili bali kadhaa

Sijui nimuache au nifanye nini kwani nimemvumilia kwa muda sasa nahitaji ushauri."

 

Mwanamke asimulia jinsi mumewe amekuwa akimcheza akisema ni mjane