Diamond atumia mabilioni kununua kisiwa cha kibinafsi Zanzibar

Muhtasari

•Kipande cha ardhi ambacho msanii huyo alinunua bado hakijajengwa na kwa sasa ni kichaka kilichojaa miti aina aina na nyasi.

•Mwandani wa mwanamuziki huyo, Baba Levo alidai kuwa kisiwa hicho kilimgharimu jumla ya Tsh1.8B. (Ksh 902,703,842).

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Siku chache zilizopita nyota wa Bongo Diamond Platnumz alikamilisha ununuzi ufukwe wa binafsi kisiwani Zanzibar.

Kwenye Instastori zake Diamond alipakia video iliyoonyesha eneo kubwa lililozingirwa na maji ya bahari la hindi ambalo anaripotiwa kununua. 

"Ilikuwa ndoto tu, Zanzibar," Diamond aliandika chini ya video hiyo.

Kipande cha ardhi ambacho msanii huyo alinunua bado hakijajengwa na kwa sasa ni kichaka kilichojaa miti aina aina na nyasi.

Baadhi ya ripoti kutoka  Tanzania zinadokeza kuwa bosi huyo wa WCB anapanga kujenga mkahawa wa kifahari pale.

Mwandani wa mwanamuziki huyo, Baba Levo alidai kuwa kisiwa hicho kilimgharimu jumla ya Tsh1.8B. (Ksh 902,703,842).

"Diamond amenunuea kisiwa Zanzibar Tsh 1, 840, 000, 000.. Mungu ni mwema sana!" Baba  Levo alisema kupitia Instagram.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya staa huyo kufichua mpango wake wa kununua ndege ya kibinafsi.

Diamond alifichua kuhusu mpango huo wake wakati akimtakia meneja wake El-Jefe Mendez heri za siku ya kuzaliwa.

"Tulinunua 2021 Rolls Royce Black Bedge Zero Kilometre mwaka jana, na tunanunua ndege ya kibinafsi mwaka huu!! hiyo ndio tafsiri ya kuwa na usimamizi bora!! Ni Siku ya Kuzaliwa ya meneja wangu Sallam Sk," Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya Sallam akiongoza shughuli ya ununuzi wa Roll Royce yake iliyofanyika mwezi Juni mwaka jana.

Picha zile zilionyesha kuwa gari hilo lilimgharimu Diamond pesa za Kiarabu AED 2, 250, 000 . (Ksh 71,200, 000/ Tsh 1.4B).