Vanessa Mdee na mumewe Rotimi wamwaga Mamilioni kununua jumba lingine la kifahari Marekani

Muhtasari

•Hivi majuzi wazazi hao wa mtoto mmoja wamenunua jumba la kifahari katika eneo la Orlando, jimbo la  Florida.

•Mapema mwaka huu Rotimi alinunua jumba lingine lenye thamani ya mamilioni kama zawadi kwa mkewe Vanessa.

Image: INSTAGRAM// VANESSA MDEE

Wanandoa maarufu Rotimi na Vanessa Mdee wameendelea kuimarika siku nenda siku rudi katika miaka miwili ya ndoa yao.

Wasanii hao wawili walianza kuchumbiana mwaka wa 2020 na hata kuanza kuishi pamoja nchini Marekani mwaka huohuo.

Hivi majuzi wazazi hao wa mtoto mmoja wamenunua jumba la kifahari katika eneo la Orlando, jimbo la  Florida.

Wawili hao walisherehekea habari hizo njema pamoja na mashabiki wao kupitia kurasa zao za Instagram.

"Densi unayosakata unaponunua jumba nyingine," Rotimi aliandika chini ya video inayomuonyesha yeye na Vanessa wakinengua kiuno mbele ya nyumba yao mpya.

Katika video nyingine msanii huyo mwenye asili ya Nigeria alionyesha mandhari mazuri yanayozingira  jumba hilo la ghorofa moja.

Miti ya mitende, nyasi maridadi na bwawa la kuogelea ni baadhi ya vitu vya kupendeza vinavyozingira nyumba  hiyo ya Rotimi na Vanessa.

Mapema mwaka huu Rotimi alinunua jumba lingine lenye thamani ya mamilioni kama zawadi kwa mkewe Vanessa.

Akiwa kwenye mahojiano Vanessa alifichua kuwa Rotimi alimzawadia jumba hilo la takriban Ksh56.8M katika msimu wa Valentines.

Siku ya wapendanao ilikuwa ya kushangaza, lakini hatusherehekei Siku ya Wapendanao kwa sababu tunapenda watu kila siku.

Lakini mwaka huu ulikuwa wa valentines kubwa kwangu, kwa sababu alininunulia nyumba mpya kabisa. Ni nyumba mpya kabisa huko Florida, yenye vyumba 6, bafu 5, eneo la kipekee, na inagharimu dola nusu milioni $500, 00. Na iko chini ya jina langu, kwa hivyo mimi ndiye mmiliki halali wa nyumba huko Amerika," Vanessa Mdee Alisema katika mahojiano na Lil Ommy.

Vanessa alibainisha kuwa wangetumia jumba hilo kama kitega uchumi kwa kuwa lipo Florida, lakini walikuwa wanaishi Atlanta Georgia wakati huo.