Hongera! Trio Mio anunua shamba yake ya kwanza akiwa na miaka 17

Muhtasari

•Msanii huyo mwenye umri wa miaka 17 alitangaza ununuzi wa kipande chake cha kwanza cha ardhi Jumamosi.

•Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanamuziki huyo kufanya bonge la shoo wakati wa maadhimisho ya Madaraka Day

Image: INSTAGRAM// TRIO MIO

Wanamitandao wameendelea kumpongeza na kumsherehekea mwanamuziki TJ Mario Kasela almaarufu Trio Mio baada ya kununua kipande cha ardhi.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 17 alitangaza ununuzi wa kipande chake cha kwanza cha ardhi Jumamosi.

Trio Mio alipakia picha inayoonyesha akiwa ameshika hatimiliki ya shamba huku mamake na akiwa amesimama kando yake.

"Mmiliki mpya wa ardhi mjini. Mkuruweng. Mungu ibariki 2022," Trio Mio aliandika chini ya picha hiyo ambayo alipakia Instagram.

Trio Mio hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu kipande chake cha ardhi wala kufichua mahali kilipo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanamuziki huyo kufanya bonge la shoo wakati wa maadhimisho ya Madaraka Day yaliyofanyika Uhuru Gardens.

Trio Mio alishirikiana na wasanii wenzake Iyanii na Femi One kutengeneza kibao 'Tunaweza' ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya kusherehekea Madaraka Day.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri wamempongeza Trio Mio kwa hatua ya kununua shamba ambayo amepiga.

@khaligraph_jones Sasa tuanze ile Mansion na hizi marupurupu za show tuimalize kufikia 2024? Unaonaje huo mpango?

@official_r.i.gg.y Cheti tunacho sasa mkurugenzi au sio.

@moisbridgian Baraka

Mapema mwaka huu msanii huyo alifichua kuwa mama yake, Sofia Irma Sakwa amekuwa akihusika pakubwa katika usimamizi wa mapato ya muziki wake.

Alifichua kuwa mbali na majukumu ya kawaida ya mamake kama mzazi, yeye pia ni meneja wake wa muziki.

"Mamangu hunipanga mara nyingi. Huwa ananipanga kuhusu masuala ya pesa, kuzisimamia. Huwa najua vile nitacheza" Trio Mio alisema akiwa kwenye mahojiano na Churchill.

Pia alisema kuwa baba yake ambaye ni mwanamuziki pia huwa anamsaidia sana katika taaluma yake hasa kwa ushauri.

"Babangu huwa ananisaidia. Huwa ananirekebisha. Anajua hayo mambo sana" Alisema.

Aliweka wazi kuwa  licha ya kwamba ana uwezo mkubwa wa kifedha, huwa hapendelei kutembea na pesa nyingi mfukoni haswa anapokuwa akielekea shuleni.