"Najivunia wewe" Harmonize afunguka sababu kuu ya kumpenda Kajala

Muhtasari

•Harmonize amedai kuwa mama huyo wa binti mmoja hurauka majogoo kila Jumapili ili kujiandaa kuenda kanisa.

•Harmonize ambaye amezaliwa katika familia ya Kiislamu ameapa kuandamana na muigizaji huyo kuenda kanisani siku moja.

Harmonize na Kajala
Harmonize na Kajala
Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Harmonize amesema kwamba anampenda sana muigizaji Kajala Masanja kwa vile yeye ni Mcha Mungu.

Harmonize amedai kuwa mama huyo wa binti mmoja hurauka majogoo kila Jumapili ili kujiandaa kuenda kanisa.

"Ndiyo maana ninampenda. Daima huwa anamuweka Mungu mbele. Yeye huamka saa kumi na mbili asubuhi kila Jumapili kwenda kanisani," Harmonize alisema kupitia Instastori zake.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide aliambatanisha ujumbe wake na picha ambayo Kajala alipakia Jumapili asubuhi alipokuwa akielekea kanisani.

Harmonize ambaye amezaliwa katika familia ya Kiislamu ameapa kuandamana na muigizaji huyo kuenda kanisani siku moja.

"Siku moja nitaenda naye kwa nyumba nzuri ya Mungu Inshalllah. Najivunia wewe," Aliandika.

Kajala alipochapisha picha hiyo yake aliwasihi watu kutokubali ushauri wa watu ambao hawawahi kupitia hali ambayo wanapitia.

"Usiruhusu mtu yeyote ambaye hajawahi kuvaa viatu vyako akuambie jinsi ya kufunga kamba zako. Jumapili njema," Kajala aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika kipindi cha siku chache ambazo zimepita muigizaji huyo amekuwa likizo katika mbuga la wanyama la Serval Wildlife.

Kajala amekuwa akirekodi matukio a ziara yake katika mbuga hilo na kuonyesha na mashabiki wake kupitia Instagram.

Picha moja ambayo ilionyesha muigizaji huyo akibusu twiga ilinasa umakini wa Harmonize. Mwanamuziki huyo alimtaja twiga huyo kuwa mwenye bahati zaidi duniani kwa kubusu mpenzi wake.

"Twiga mwenye bahati zaidi duniani.Karibu kumbusu mwanamke wangu. Kuna mtu aliniambia boss lady yupo likizo huko. Furahia mama ni wakati wako," Harmonize aliandika chini ya picha hiyo.