Kiasi cha pesa alichoibiwa Jalang'o na waliokuwa wafanyikazi wake

Muhtasari
  • Hii ni baada ya waliokuwa wafanyakazi wake kuiba pesa, kutoka kwa gari walilokuwa wanaosha na kutoroka
Jalango
Jalango
Image: Hisani

Wikendi iliyopita haikuwa ya furaha kwa mwaniaji ubunge wa Lang'ata, mcheshi na mtangazaji Jalang'o.

Hii ni baada ya waliokuwa wafanyakazi wake kuiba pesa, kutoka kwa gari walilokuwa wanaosha na kutoroka.

Habari hizo zilitangazwa na Jalang'o,ilhali hakufichua kiasi cha pesa walichoiba, huku akitoa zawadi kwa mtu yeyote atakaye onyesha walipokuwa wafanyakazi hao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Jalang'o alisema kuwa;

"Eli na Litiema wako mbioni, leo asubuhi waliiba pesa kwenye gari walilokuwa wakiosha nyumbani, simu zao hazipo na wanakimbia na familia zao. Ukiwaona tafadhali wasiliana 0722915337 au toa taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu nawe Zawadi ya 100k kwa taarifa yoyote itakayopelekea kukamatwa kwao."

Rafikiye  Jalang'o, Billy Miya alidai kuwa wafanyikazi hao wawili walitoroka na KSh 2.5 milioni.

"Weuh! Shetani ni mtu mubaya sana.Unahustle na boss wako for more than 4 years, ile mwaka anaenda kuingia bunge shetani anakudanganya unaiba 2.5M.Yaani si mungesubiri boss aingie Bunge mukuwe mafutani.Jamani tupige ripoti polisi Au piga 0722 717 159.Pole sana Jalango Mwenyewe itakua sawa.Uzuri alitupeleka moja kwa moja hadi kwao kupitia social media.Over to you DCI Kenya,"Billy alifichua.