"Nakupenda na kukuheshimu" Jux na Huddah wafunguka kuhusu uhusiano wao halisi

Muhtasari

•Juma Jux alimsaidia mwanasoshalaiti huyo kuzindua bidhaa zake za 'Rich Beauty' nchini Tanzania.

•Jux alimpongeza Huddah kwa hatua aliyopiga huku akimhakikishia kuhusu heshima na upendo wake mkubwa kwake.

Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Juma Jux na mwanasoshalaiti Huddah Monroe kutoka Kenya wamedokeza kuwa uhusiano wao sio wa kimapenzi.

Wasanii hao wawili ambao siku za hivi majuzi wamedhaniwa kuwa kwenye mahusiano walifichua hayo wakati Huddah alipotembelea duka la nguo la African Boy lake Jux.

Jux pia alimsaidia mwanasoshalaiti huyo kuzindua bidhaa zake za 'Rich Beauty' nchini Tanzania. Alipokuwa anataoa maelezo kuhusu bidhaa zake, Huddah alifichua kuwa uhusiano wake na Jux ni wa kirafiki tu.

"Juma mchezo wake sijui. Sisi ni marafiki tu," Huddah alisema.

Wawili hao hata hivyo waliibua shaka kubwa kuhusu uhusiano wao baada ya kubusu hadharani bila wasiwasi wakati wakifanyia lipstick ya Huddah majaribio.

"Lipstick yake haitoki rangi. Mara nyingi huwa namwambia tujaribu bidhaa zake. Zingine sijafika kuzijaribu lakini nitaziangalia. Yeye ni rafiki yangu," Jux alisema baada ya kumbusu Huddah.

bidhaa ambazo Huddah alizindua nchini Tanzania ni pamoja na vipondozi, dawa za nguvu za kiume na zile za kike.

Jux alimpongeza Huddah kwa hatua aliyopiga huku akimhakikishia kuhusu heshima na upendo wake mkubwa kwake.

"Hakuna jambo zuri kama watu wa karibu, wawe marafiki au wapenzi kupeana support. Hongera Huddah kwa kuzindua bidhaa zako nchini Tanzania. Wewe ni mpambanaji, Nakupenda na kukuheshimu. Endelea kusukuma," Jux alimwambia mwanashalaiti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Huddah alizuru Tanzania wiki jana na kupokewa na Jux katika uwanja wa ndege kisha wakaelekea nyumbani kwake.

Wawili hao walionekana wakijivinjari pamoja katika maeneo mbalimbali na kuongeza hisia kuwa huenda wanachumbiana.