Diamond Platnumz awasili nchini saa chache baada ya Zari kuwasili

Muhtasari
  • Diamond Platnumz awasili nchini saa chache baada ya Zari kuwasili 
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Wasafi Diamond Platnumz aliwasili nchini Kenya siku ya Jumatano saa chache baada ya Zari Hassan naye kuwasili.

Diamond hakuweka wazi ziara yake nchini, bali aliweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa Nairobi,katika mkahawa wa Cip LOunge.

Mwanasosholaiti huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumatano asubuhi na kupokelewa na wenyeji wake Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Zari alisema kuwa yuko nchini Kenya kwa shughuli za kibiashara na atazindua jumba jipya la kifahari lililoundwa na kampuni ya Fine Urban Construction & Interiors Ltd.

"Niko hapa kufichua jumba ambalo limesanifiwa na Fine Urban Construction and Interiors na ni moja ya nyumba za nje ya dunia hii ambazo usingetarajia katika Afrika Mashariki. Kwa hiyo niko hapa kufichua kazi zao,

Natakiwa kufanya kazi na mke wa Gavana (Mike Sonko) na tunatakiwa kutembelea nyumba za watoto. Mimi kuja Kenya na kutojishughulisha na hiyo isingekuwa ziara ya Zari. Napenda chakula cha Kenya, huo ni ugali. nyama choma na sukuma wiki,"Alizungumza Zari.

Zari atahudhuria karamu katika klabu ya XS Millionaires leo.