Wanaume huninunulia magari na nyumba,sijawahi kuwa single maishani mwangu-Huddah

Muhtasari
  • Pia aliweka wazi kwamba hatawahi wapakia watoto wake au mume wake mitandaoni
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Huddah Monroe

Mwanasosholaiti HUddah hataacha kuwashangaza mashabiki wake,hasa inapokuja katika uhusiano wa kimapenzi na biashara.

Huddah amekuwa akivuma katika siku chache zilizopita hii ni baada ya uvumi kuenea kwamba anamchumbia mwanamuziki wa Tanzania Juma Jux.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mwanasosholaiti huyo amesema kwamba maishani mwake hajawahi kuwa Single kama vile wengi wanavyofikiria.

"Jambo la kwanza siwezi kaa bila mwanamume,wanaume wameninunulia magari na manyumba sijawahi kuwa single maishani mwangu sijui huwa wanafanya aje kwa mtu kama mimi," HUddah alisema.

Huddah na Jux ata hivyo waliibua shaka kubwa kuhusu uhusiano wao baada ya kubusu hadharani bila wasiwasi wakati wakifanyia lipstick ya Huddah majaribio.

"Lipstick yake haitoki rangi. Mara nyingi huwa namwambia tujaribu bidhaa zake. Zingine sijafika kuzijaribu lakini nitaziangalia. Yeye ni rafiki yangu," Jux alisema baada ya kumbusu Huddah.

Bidhaa ambazo Huddah alizindua nchini Tanzania ni pamoja na vipondozi, dawa za nguvu za kiume na zile za kike.

Jux alimpongeza Huddah kwa hatua aliyopiga huku akimhakikishia kuhusu heshima na upendo wake mkubwa kwake.

"Hakuna jambo zuri kama watu wa karibu, wawe marafiki au wapenzi kupeana support. Hongera Huddah kwa kuzindua bidhaa zako nchini Tanzania. Wewe ni mpambanaji, Nakupenda na kukuheshimu. Endelea kusukuma," Jux alimwambia mwanashalaiti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Pia aliweka wazi kwamba hatawahi wapakia watoto wake au mume wake mitandaoni.