Nilikuwa nimeolewa kwa miaka 4-Huddah Monroe afichua siri yake kubwa

Muhtasari
  • Huddah alifichua kuwa alikuwa ameolewa kwa muda si mmoja bali miaka minne akiwa na umri mdogo wa miaka 19 na mwanamume ambaye hakufichua jina lake
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Huddah Monroe aliamua kufichua na kufunguka kuhusu maisha yake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akiwafahamisha mashabiki mambo ambayo hawakuwa wanayajua kumhusu.

Mjasirimali huyo anafahamika sana mitandaoni kwa ajili ya biashara yake.

Mjasiriamali aliyefanikiwa alichukua hadithi zake za insta kushiriki kile alichotaja kuwa siri yake kuu.

Huddah alifichua kuwa alikuwa ameolewa kwa muda si mmoja bali miaka minne akiwa na umri mdogo wa miaka 19 na mwanamume ambaye hakufichua jina lake.

Haikuwa hivyo tu,  aliongeza kuwa wawili hao hawakupata watoto kwa sababu mwanamume wake alikuwa mraibu wa dawa za kulevya.

"Nilikuwa kwenye ndoa kwa miaka 4 @ 19, hatukuwa na mtoto na tukaachana kwa  sababu mwanaume alikuwa mlevi wa dawa za kulevya! Sikuwa maarufu kwa hivyo sikuhitaji kuitangaza! So naongea kwa uzoefu. Si mzaha nyinyi nyote! Usiku mwema! Hiyo ndiyo siri yangu kubwa." Soma chapisho la Huddah.

Ufichuzi wa Huddah unajiri siku chache baada ya kukiri kuchumbiana na mwanamume Mtanzania akisema wawili hao walikuwa wakipanga kufunga ndoa hivi karibuni.

Mrembo huyo alikuwa akizungumza kwenye mahojiano na vyombo vya habari vya Tanzania lakini alikataa kutaja mtu huyo wa ajabu ni nani.

"Hivi karibuni,namchumbia  mtu nchini Tanzania," alisema.