'Waganga wenu hawaniwezi,'Willy Paul awaambia wasanii wenzake

Muhtasari
  • Willy Paul alisema kuwa wanamuziki wanatembelea waganga kwa jina au kujaribu kumfanya ashindwe kimuziki na hata kumchafua
Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Mmoja wa msanii maarufu na mwenye utata nchini Willy Paul amezua gumzo tena mitandaoni.

Willy Paul ambaye amekuwa akivuma mitandaoni wiki hii baada ya kujivunia maelfu ya pesa mtandaoni na kujigamba jinsi alivyo tajiri, sasa anadai wasanii wa Kenya wanatumia nguvu za giza  kumpiga vita.

Akiongea kupitia kwa video inayomuonyesha akitengeneza gari kando ya barabara moja kuu jijini Nairobi, Willy Paul alisema kuwa wanamuziki wanatembelea waganga kwa jina au kujaribu kumfanya ashindwe kimuziki na hata kumchafua.

"Wasanii achaneni na Mimi waganga wenyu hawaniwezi, niko mpweke leo na sio kwa sababu ya mwanamke, mwanamke hawezi nianya niwe mpweke,kwani gari itashinda kupata puncture 

Hamuwezi niua na sitawahi kufa," Willy Paul Alizungumza kwenye video.