logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tafuta hela utajua msamaha huombwa vipi- Harmonize awashauri wanaume

Amewakosoa vikali wanaume wanaowataka wake zao kujitafutia hela.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 June 2022 - 06:12

Muhtasari


•Amewakosoa vikali wanaume wanaowataka wake zao kujitafutia hela huku akiwaarifu kuwa ni jukumu lao kuwashughulikia.

•Kulingana na msanii huyo, hatua ya kuomba msamaha huwa rahisi zaidi wakati mwanaume anapomshughulikia mpenziwe kihela.

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amewashauri wanaume kutafuta hela ili kuboresha uhusiano kati yao na wapenzi wao. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amesema wanawake wanafaa kuruhusiwa kupumzika na kushughulika na uzazi wala sio kufanya kazi.

Amewakosoa vikali wanaume wanaowataka wake zao kujitafutia hela huku akiwaarifu kuwa ni jukumu lao kuwashughulikia.

"Tafuta hela watoto wa kike tuwaache watuzalie kwa uchungu. Hivi unapata wapi ujasiri wa kumwambia mtoto wa kike afanye kazi? Ajitumie nini sasa au wewe unajituma kwa ajili ya nani?" Harmonize alisema.

Kulingana na msanii huyo, hatua ya kuomba msamaha huwa rahisi zaidi wakati mwanaume anapomshughulikia mpenziwe kihela.

Alishauri kwamba mwanaume anapaswa kutumia hela kumfanya mwanamke asahau makosa yake badala ya kumtumia jumbe nyingi za kuomba msamaha.

"Tafuta hela ukishakuwa nazo ndio utajua msamaha unaombwa aje. Hizo SMS zako unamjazia WhatsApp unazidi kumuumiza na kumkumbusha machungu. Mfanye asahau babuu. Mpeleke katika dunia nyingine," Alisema. 

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alikuwa anazungumzia kibao chake cha hivi majuzi 'Deka' ambacho alitumia kuwashauri wanaume kuwadekeza wapenzi wao na vitu wanavyopenda kila wakati wanapotaka msamaha ama jambo fulani kutoka kwao.

Haya yanajiri wiki chache tu baada yake kumwaga mamilioni ya pesa katika juhudi za kumuomba msamaha mpenzi wake Kajala Masanja.

Harrmonize alimnunulia muigizaji huyo magari mawili aina ya Range Rover, mkufu wa dhamani, na zawadi zingine maalum katika juhudi za kumshawishi warudiane.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved