Pritty Vishy ajibu madai ya Stivo kuwa alitoka kimapenzi na wanaume zaidi ya 50

Muhtasari

•Stivo alidai kwamba alifahamu kuwa Pritty Vishy hakuwa mwaminifu ila akaendelea kustahimili huku akimuomba abadili mienendo.

•Vishy amesema Stivo alikosa kumwamini na angepatwa na wasiwasi mwingi kila baada ya kumuona akitembea na mwanaume yeyote barabarani.

Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Image: SCREENGRAB// MUNGAI EVE

Hatimaye Pritty Vishy amejibu madai ya aliyekuwa mpenziwe Stivo Simple Boy kuwa alitoka kimapenzi na zaidi ya wanaume 50 walipokuwa wanachumbiana.

Simple Boy akiwa katika mahojiano ya hivi majuzi alidai kuwa mpenzi huyo wake wa zamani alikuwa anamcheza mara kwa mara.

Alidai kwamba alifahamu kuwa Pritty Vishy hakuwa mwaminifu ila akaendelea kustahimili huku akimuomba abadili mienendo.

"Mimi nilinyamazia tu. Nilikuwa nikimwambia  kama ananipenda cha kweli awachane na hayo mambo yake. Nilimwambia akuwe na mtu mmoja ili tufunge ndoa. Lakini haeleweki jameni," Alisema katika mahojiano na Oga Obinna.

Vishy akijibu madai hayo amesema Stivo alikosa kumwamini na angepatwa na wasiwasi mwingi kila baada ya kumuona akitembea na mwanaume yeyote barabarani.

"Shida ya Stivo ata akiniona kwa barabara nikitembea na mjomba wangu jioni angekuja aniambie alisikia nilikuwa natembea na mwanaume. Nilishangaa kwani sifai kutembea na watu kwa sababu nachumbiana na yeye.Huyo ni mpenzi sumu," Vishy alisema katika mahojiano na Obinna.

Kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 alidai ikiwa Simple Boy alifahamu kuwa hakuwa mwaminifu basi angekatiza mahusiano yao.

Vishy hata hivyo alikiri kuwa alijihusisha kwenye mahusiano na wanaume kadhaa tajiri wenye umri mkubwa wanaojulikana kama 'wababaz'

Alifichua kuwa aliwahi kuchumbiana na 'mubabaz' mmoja mashuhuri ambaye alikutana naye katika harusi.

"Nilikutana naye harusini. Alikuwa MC," Alisema.

Aidha kipusa huyo alidai kuwa pia Stivo alikuwa anamcheza na wanadada kadhaa ambao alikuwa akitaniana nao kwenye simu.

"Jambo hilo hadi ilileta shida. Ilikuwa karibu tupigane. Ni kama alikuwa ananicheza. Mimi nilikuwa najua tulikuwa kwenye mahusiano lakini pia huko nje anachumbiana," Alisema.

Vishy ameshikilia kuwa hakuwahi kushiriki tendo na ndoa na Stivo wakati wa mahusiano yao.