Sitawahi piga kura-Huddah Monroe akiri

Muhtasari
  • Pia aliwahimiza wananchi kuwa na amani wakati wa uchaguzi na kuepuka kujihusisha na vurugu
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Huddah Monroe

Mwanasosholaiti maarufu nchini Huddah Monroe kupitia ukurasa wake wa instagram amewashangaza wengi baada ya kufichua kwamba hajawahi piga kura.

Mwanasosholaiti huyo kwenye Instagram yake alisema hatapiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao utakaopangwa kufanyika Agosti mwaka huu.

Kulingana na Huddah, yeye ni mlipa kodi tu anayeishi maisha yake na kutazama pembeni. Hata hivyo, alisema kuwa anatetea watu kupiga kura.

"Sijawahi kumiliki kadi ya wapiga kura. Sijawahi kupiga kura. Ninatetea upigaji kura lakini sitawahi kupiga kura. Sarakasi sio yangu. Ni mlipakodi anayeishi maisha yake akitazama pembeni. Na kutajirisha familia za viongozi wenu. ili waendelee kuishi kwa wingi."

Pia aliwahimiza wananchi kuwa na amani wakati wa uchaguzi na kuepuka kujihusisha na vurugu.

"Sijali nani atakaye shinda ajenda zao haziwahi saidia familia yangu wala kunisaidia ndio maana inaniuma nikiona watu wakipigana kwa ajili ya watu ambao hawawajali na wala kusaidia familia yao, tuweni na amani."

Aidha amewahimiza wanasiasa wasilete vurugu endapo watashindwa kwenye uchaguzi mkuu.