Eko Dydda afunguka mipango yake ya kisiasa

Muhtasari

•Dydda alisema wafuasi wake kutoka wadi ya Mathare Kusini wanataka awanie kiti cha MCA kwa kuwa ako na roho ya kusaidia watu.

•Ameahidi kuwa mtu wa karibu na wakaazi wa Mathare kabla na hata baada ya  kuchaguliwa kuwa MCA wao.

Image: INSTAGRAM// EKO DYDDA

Mwimbaji wa nyimbo za injili Eko Dydda amejitosa kwenye ulingo wa siasa.

 Akiwa kwenye mahojiano na Mpasho, Dydda alisema wafuasi wake kutoka wadi ya Mathare Kusini wanataka awanie kiti cha MCA kwa kuwa ako na roho ya kusaidia watu.

Yeye ni msanii  wa pili kutoka Mathare kuingia siasani baada ya Kevin Kioko almaarufu Bahati ambaye anawania kiti cha ubunge cha Mathare kutumia tikiti ya Jubilee.

Dydda aliweka wazi kuwa  yeye ni Mcha Mungu na kudai kuwa Mungu ndiye aliyeongea naye kupitia wufuasi wake kuwania kiti cha MCA Mathare.

Alisema mtindo wake wa siasa sio kama wanasiasa wengine ambao huleta fujo wakati wa kampeni zao. Alidai kuwa yeye anaamini kuwa kiongozi huchaguliwa na Mungu na si lazima ujifanye mbabe ndivyo uonekane mwanasiasa.

Aliongezea kuwa mwanasiasa kamili ni Yule ambaye sera zake ziko kamilifu na pia uvutia watu, na hizo sera lazima zikue ahadi za ukweli bali si kuwa danganya hili wakupigie kura.

Baadhi za hoja katika manifesto yake ni kuunganisha watu wote na kutetea haki zao. Ameahidi kuwa mtu wa karibu na wakaazi wa Mathare kabla na hata baada ya  kuchaguliwa kuwa MCA wao.

‘Ofisi yangu itakua tu hapa Mathare, mtu yeyote ambaye anataka kuniona atakuwa ananipata hapa Mathare,sitakuwa kama MCAs wengine ambao wakishachaguliwa wanapotea, kama ni basari mimi nitakuwa nakupatia tu kwa ofisi’Eko Dydda alisema

Eko dydda alikashifu tabia za wanasiasa ambao hawataki kuwajibikia jukumu zao wakishakabidhiwa  kazi na wananchi.

‘Baadhi ya wanasiasa wakishaingia katika ofisi, wananchi wakiwapigia simu hawachukuwi, kuonana na yeye ni shida, kupewa basari ni shida, lakini wakati walikuwa wanatafuta kura kutoka kwa wananchi walikuwa wanapatikana kila wakati, mimi sitakuwa kama wao nitapatikana kila wakati’

Lengo lake kuu alisema ni kuhakikisha kuwa watu wamepata risilimali kwa urahisi  bila kuteseka, kwasababu kazi yake kuu kama MCA ni kuhakikisha kuwa amefanyia watu wa Mathare kazi kwa ufasaha.

Pia alihakikishia mashabiki kuwa kando ya kuwa mwanasiasa ataendelea na kazi yake ya usani, maanake anajua jinsi atakapo hakikisha kuwa anahudumia wananchi na pia kuendeleza kazi yake ya usani.