Nilipatwa na upweke nikiwa kwenye ndoa-msanii Size 8 afichua

Muhtasari
  • Alieleza kuwa wanawake wanafikiri hatimaye watakuwa na furaha watakapoolewa
Image: INSTAGRAM// DJ MO

Msanii wa nyimbo za injili na muhubiri Size 8 sio mgeni vinywani mwa watu wengi au mgeni mitandaoni kwani anafahamika sana kupitia bidii ya kazi yake.

Size 8 amezungumza kuhusu kukumbana na upweke mapema katika ndoa kwa sababu ya kutarajia mengi kutoka kwa mwanamume wake.

Alieleza kuwa wanawake wanafikiri hatimaye watakuwa na furaha watakapoolewa.

Alikuwa akizungumza na YouTuber Priscilla Ndanu kwenye sehemu ya PourItout,

“Nahisi kwa hakika wanawake wengi wana tatizo hilo, nilikuwa na tatizo hilo katika ndoa yangu ya utotoni nikijiuliza huku kunaendaga aje.

Nilipata upweke katika ndoa nilipoanza hasa nilipopata ujauzito,Unajua mimi na mume wangu tulikuwa tukiishi pamoja wakati wote basi nilipopata ujauzito na ikabidi nibaki nyumbani katika masuala ya kitandani na ujauzito nilijihisi mpweke.”

Aliongeza kuwa;

"Nilikuwa na matarajio haya ya kuchekesha kwamba nilikuwa naingia kwenye ndoa kwamba mtu huyu atatumiwa na Mungu kunitimizia

"Wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa kutokana na upweke mtupu."