Nilimpenda sana Lavalava kuliko Rich Mavoko,Lulu Diva akiri

Muhtasari
  • Nilimpenda sana Lavalava kuliko Rich Mavoko,Lulu Diva akiri
  • Nini haswa kimekosa katika uhusiao wa kimapenzi katika karne hii ya sasa?
Lulu Diva
Lulu Diva
Image: INSTAGRAM

Unaweza kuwa unajiuliza mbona watu wengi hawamo kwenye uhusiano wa kimapenz au walikata tamaa baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kwanza.

Jibu ni kuwa wengi walivunjika moyo kwani walikuwa wamewapeda wenzi wao kwa moyo wao wote lakini wenzi wao hawakuyaona hayo waliishia kuwasaliti.

Sio kisa kimoja au viwili bali tumewaona watu mashuhuri, wasanii,waigizaji,wakipendana na baada ya muda wanaachana, huku wakilaumiana.

Nini haswa kimekosa katika uhusiao wa kimapenzi katika karne hii ya sasa?

Ni wengi ambao wamekwa wakijiuliza haya, huku asilimia kubwa ikisema kwamba ni uaminifu,ndoa,uhusiano bila uaminifu sio uhusiano tena.

Mwigizaji na mwanmuziki kutoka Tanzania Lulu Diva ameweka wazi ni ex yupi wake alikuwa anampenda sana

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafitv  Lulu alikiri kwamba alimpenda sana staa wa bongo Lavalava.

"Kati ya Rich Mavoko na Lavalava ulimpenda nani sana,"Lulu aliulizawa.

"Nilimpenda sana Lavalava,"Msaniii huyo alijibu kwa ujasiri.

Msanii huyo aliweka wazi kwama haogopi mtu yeyote kwa chcochote anchofanya masihani mwake;

"Siogopi MTU wala KITU!...Sababu Nikikosa Mkate kwa kuona Aibu hakuna ATAKAENILETEA Mkate MEZANI kinywa changu kinausubiri mkono Uufikie, basi siwezi kusubiri hadi WATU waniamulie...Huyu ndo mimi.."